1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vimezuka tena mashriki ya kati

25 Agosti 2011

Mapambano kati ya Israel na wanamgambo katika ukanda wa Gaza yalizuka tena hapo jana jioni na mapema hii leo licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano hayo

https://p.dw.com/p/12NRB
Athari za mripuko GazaPicha: dapd

Mapambano hayo yamesababisha vifo vya wapalestina 5 na kuwajeruhi watu 30.

Luftangriff auf Gazastreifen Israel
Yaliosalia baada ya miripukoPicha: picture alliance/dpa

Kwa mujibu wa msemaji wa huduma za dharura, Adham Abu Selimiya, miongoni mwa watu hao watano waliouawa, wawili walikuwa wanamgambo wakiisilamu wa kundi la Islamic Jihad.

Ndege za kivita za Israeli zilifanya mashambulio matatu katika pwani ya eneo hilo hapo jana usiku. Na Abu Selmeya amesema Mpalestina mmoja aliuawa na wengine 10 walijeruhiwa wakati ndege ya Israel ilipofyatua mripuko ulioanguka katika ukumbi wa michezo hii leo asubuhi katika eneo la Beit Lahia kaskazini mwa ukanda wa Gaza.

Israel Gaza Palästinenser Raketenbeschuß von Beersheba
Picha: picture-alliance/Photoshot

Maafisa wa afya wa Palestina wamesema pia mwanamgambo mmoja wa kiislamu aliuawa na wengine wawili walijeruhiwa hapo jana usiku wakati mripuko mwingine uliofyatuliwa na Israel ulipolilenga kundi la wanamgambo katika mji wa Gaza.

Ndege hizo za kivita za Israel pia zilishambulia njia za chini kwa chini zilizopo katika mji wa Rafah kusini mwa ukanda wa Gaza karibu na mpaka wa Misri.

Mashambulio hayo matatu yalifanyika kujibu mashambulio ya roketi ya Palestina yaliofanywa kutoka Gaza dhidi ya eneo la kusini mwa Israel.

Sehemu ya kundi la Isalmic Jihad lililojihami, Saraya al Quds, limedai kuhusika na mashmabulio matano ya roketi kutoka ukanda wa Gaza dhidi ya miji iliyopo kusini mwa Israeli, Ashkelon na B'er Sheba. Hakuna visa vyovyote vilivyoripotiwa vya watu kujeruhiwa.

Raketenangriff auf Israel
Shambulio katika mji wa B'er ShebaPicha: dapd

Kundi lililojihami la kutetea kujitenga kwa Palestina, awali lilidai kuhusika na mashambulio mawili ya roketi kutoka ukanda wa Gaza dhidi ya eneo hilo la kusini mwa Israeli.

Kituo cha redio cha Israeli kimemnukuu msemaji wa jeshi nchini humo aliyesema ndege za kivita za nchi hiyo zilifanya mashambulio kadhaa katika ukanda huo wa Gaza.

Ongezeko la hivi karibuni la vurugu, linajiri baada ya Israeli na makundi ya wanamgambo Gaza kufikia makubaliano ya kusitisha mashambulio baada ya mashambulio makali ya siku tatu ambapo wapalestina 15 na waisraeli wawili waliuawa.

Luftangriff auf Gazastreifen Israel
Picha: picture alliance/dpa

Hii leo waziri wa ulinzi wa ndani Israeli, Matan Vilnai amekiambia kituo cha radio cha jeshi kuwa nchi hiyo itaendelea kuishambulia Islamic Jihad iwapo litaendelea na harakati zake za kigaidi dhidi ya israel.

Alieleza kuwa Kundi la Hamas linajihadhari kwa kuwa ni kwa manufaa yake kuwa vurugu hizi zinamalizika.

Waziri wa upelelezi Dan Meridor amekiambia kituo cha radio ya umma kuwa Israeli ipo tayari kuheshimu makubaliano ya kusitisha mashambulio iwapo tu patakuwa na utulivu mpakani.

Mwandishi: Maryam Abdalla/Dpae/Afpe
Mhariri: Yusuf Saumu