1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita Gaza- Mashambulizi bado yaendelea

Eric Kalume Ponda16 Januari 2009

Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa chama cha Hama ameuawa leo kufuatia mashambulizi yaliyoendelezwa na wanajeshi wa Isarael karibu na mji wa Gaza.

https://p.dw.com/p/GZiB
Wanajeshi wa Israel wanaoendeleza mashambulizi Gaza.Picha: picture alliance / landov

Baada ya mashambulizi makali ya hapo jana yaliyosambaa hadi makao ya umoja wa mataifa na jengo linalotumiwa na waandishi wa habari wa Kigeni katika eneo la Tal Al Hawa mjini Gaza , wanajeshi hao leo walionekena kurudi nyuma huku makombora ya Hamas kwa mara ya kwanza kabisa yakikosa kusikika katika ardhi ya Israel.


Hii imetoa sura kwamba huenda juhudi za kutafuta amani katika kanda hiyo zinaelekea kufanikiwa

Mashambgulizi ya leo yalilenga vituo 40 vinavyodaiwa kuwa ghala la zana za Hamas ambapo waziri wa mambo ya ndani wa Chama cha Hamas, Said Siam, aliuawa jana huku mashambulizi hayo yakiingia siku yake ya 21.


Siad Siama ni miongoni mwa viongozi wa chama hicho cha Hamas waliowatimuwa maafisa wa usalama waliokuwa wakimuunga mkono Rais Mahmud Abas kutoka eneo hilo la Gaza.


Miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa hivi leo ni pamoja na msikiti unaodaiwa ni maficho ya wafuasi wa Hamas.

Hakuna habari zozote zilizotolewa kuhusu idadi ya watu waliouawa wakati wa shambulizi hilo la usiku.


Kuna habari kuwa mashambulizi hayo yalipungua leo, hali iliyotoa nafasi kwa wakaazi wa eneo la Tal Al Hawa waliolazimika kutoroka mashambulizi makali ya hapo jana kurejea eneo hilo ambako vifusi vya majengo yaliyoharibiwa vilizagaa kila mahali. Miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa ni pamoja na makao ya mashirika ya Umoja wa mataifa.


Rais wa Israel, Shimon Peres, amsema huenda mashambulizi hayo sasa yanaingia awamu yake ya mwisho na huenda yakafika kikomo hivi karibuni.


Hii ni baada ya Wafuasi wa chama cha Hamas leo kujizuia kuvurumisha makombora katika ardhi ya Israel hali inayotoa mwangaza kwamba huenda wafuasi hao wanataka kuzingatiwa mpango wa amani unaoongozwa na Misri.


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayefanaya ziara yake katika eneo hilo la Mashariki ya Kati kusukuma juhudi za kukomeshwa kwa vita hivyo, anaitaka Israel ikomeshe mashambulio hayo na kuridhia juhudi ya kuleta amani katika eneo hilo.


Mjumbe wa Israel kwenye mpango wa amani unaoongozwa na Misri, Amos Gila, anatarajiwa kuiarifu serikali yake kuhusiana na maependezo yaliyomo kwenye mpango huo baada ya kufanya mashauriano na mpatanishi mkuu aliyeteuliwa na Misri, Omar Suleima, mjini Kairo.

Baraza la usalama la Israel linatarajiwa kutoa uamuzi kuhusiana na mapendekezo yaliyotolewa na wafuasi wa chama cha Hamas kwenye mpango huo hivi leo au kesho jumamosi.


Kwenye mapendekezo yao, Hamas wamekubali kusitisha vita kwa muda wa mwaka mmoja ambao unaweza kuongezwa kwa kuzingatia hali ilivyo katika eneo hilo.


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Israel, Tzipi Livni, anatarajiwa kusafiri hadi Marekani hivi leo kufanya mashauri na Rais George W Bush kuhusiana na mpango huo wa amani.


Mpango huo unataka kukomeshwa mara moja kwa mashambulizi, kuondoka kwa Israel katika ukanda wa Gaza, na pia kufunguliwa maeneo yote ya mpakani.


Zaidi ya Wapalestina 1,100 wameuwa huku wengine 4,500 wamejeruhiwa, tangu vita hivyo vianze. Jumla wa wanajeshi 10 na raia watatu wa Israel wameuawa .