Vita-Gaza- Ilitenda uhalifu wa kivta yadai UM | Matukio ya Kisiasa | DW | 23.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Vita-Gaza- Ilitenda uhalifu wa kivta yadai UM

Serikali ya Israel imetangaza kwamba inajiandaa kwa uwezekano wowote wa maafisa wake wa kisiasa na kijeshi kushtakiwa kwa madai ya uhalifu wa kivita.

Mabomu ya Israel yanayodaiwa kuwa na kemikali ya Fosiforasi yakishambulia Gaza.

Mabomu ya Israel yanayodaiwa kuwa na kemikali ya Fosiforasi yakishambulia Gaza.

Hatua hii imetokea kufuatia ushahidi unaotolewa na Umoja wa mataifa kwamba Israel ilikiuka sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu wakati wa mashambulio yake dhidi ya chama cha Hamas katika ukanda wa Gaza.


Shirika la Umoja wa Mataifa linasema kwenye ripoti yake kwamba kunaushahidi wa kutosha kwamba Israel ilitenda uhalifu huo na panahaja ya kubuniwa tume huru kuchunguza visa hivyo.


Ripoti iliyokusanywa na mjumbe maalum wa shirika la kutetea haki za binadamu la Umoja huo Richerd Falk, Israel ilikiuka sheria hizo kwa kuwazuia raia kuondoka eneo la vita mbali na kutumia mabomu yenye kemikali ya Fosiforasi katika maeneo ya makaazi. Aidha Israel inashtumiwa kwa kutumia nguvu za kijeshi kupita kiasi katika maeneo hayo ya makaazi.


Richard Falk ambaye pia ni myahudi, anasema kuwa , raia wote wa Gaza walizuiliwa mateka wakati wa mashambulio hayo, huku Israel ikishambulia kila eneo ikiwemo misikiti,kambi za wakimbizi na makao ya mashirika ya misaada ya binadamu,badala ya kuelekeza mashambulizi yao katika eneo lililokuwa likitumiwa kuvurumisha makombora ya maroketi.


Hivyo basi kwa kuzingatia azimio la Umoja wa mataifa na sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu, Israel haikuwa na sababu za kisheria kufanya hivyo kwa kisingizio cha kuwalinda raia wake.


Madai haya sasa yameiweka Israel katika hali ya kujiandaa kupambana na mkono wa sheria iwapo itashtakiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu. Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert tayari amemteua Waziri wa sheria Daniel Friedmann kuongoza kamati maalum itakayobuniwa kushughulikia madai hayo. Kamati hiyo inatarajiwa kuanza kazi wiki ijayo.


Kulingana na ripoti za mashirika ya kutetea haki za binadamu katika eneo hilo la Gaza, zaidi ya watu 1,3000 waliuawa na wengine 5,000 kujeruhiwa wakati wa vita hivyo vilivoanza disemba 27 mwaka uliopita. Miongoni mwa idadi hiyo, asilimia 70 ni raia.


Kiongozi wa mashirika ya huduma za binadamu ya umoja wa mataifa katika eneo hilo John Holmes ametaka maeneo ya mipakani yafunguliwe ili kutosa nafasi ya kujenga upya eneo hilo la Gaza.


Leo ni siku ya sita tangu pande hizo mbili zitangaze hatua ya kusimamisha mashambulio, ingawa Israel inaonye kuwa itaishambulia Gaza endepo wafuasi wa Hamas watavurumisha makombora baada ya muda huo kumalizik


Ponda/Reuters


 • Tarehe 23.01.2009
 • Mwandishi Eric Kalume Ponda
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GenF
 • Tarehe 23.01.2009
 • Mwandishi Eric Kalume Ponda
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GenF
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com