Vita Baridi vimekwisha ..Urusi sio adui yetu! | Matukio ya Kisiasa | DW | 05.06.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Vita Baridi vimekwisha ..Urusi sio adui yetu!

Rais George W. Bush wa Marekani leo amejaribu kumtuliza Rais Vladimir Putin wa Urusi juu ya mipango ya Marekani ya kuweka makombora ya kujihami Ulaya ya Mashariki kwa kusema kwamba Urusi haina haja ya kuhofia kitu.

Rais George W. Busha akizungumza na Rais Vackav Klaus wa Jamhuri ya Czech mjini Prague tarehe 5 mwezi wa Juni 2007.

Rais George W. Busha akizungumza na Rais Vackav Klaus wa Jamhuri ya Czech mjini Prague tarehe 5 mwezi wa Juni 2007.

Akizungumza katika mkesha wa mkutano wa viongozi wa nchi za Kundi la Mataifa Manane G8 lenye maendeleo makubwa ya viwanda duniani mji Prague Jamhuri ya Czek Bush amesema vita baridi vimemalizika.

Mohamed Dahman na ziara ya Bush nchini Czeck alitaka kuondowa wasi wasi kwamba nchi zenye kushirikiana na Marekani juu ya mpango huo wa makombora ya kujihami zitakuja kunaswa katika mvutano na Urusi.

Kiongozi wa Urusi Vladimir Putin alitowa majibu makali kuhusiana na mpango huo wa Marekani wa makombora ya kujihami katika Jamhuri ya Czech na na Poland na kuonya kwamba Urusi nayo itaweka makombora yake kulenga Ulaya kama ilivyofanya wakati wa vita baridi iwapo serikali ya Marekani itaendelea na mpango wake huo.

Kuongezeka kwa hali ya mvutano kati ya Urusi na Marekani kwenye mkesha wa mkutano wa kundi la Mataifa Manane tajiri kabisa duniani unaoanza hapo kesho mjini Heillegendam nchini Ujerumani kumezusha wasi wasi miongoni mwa washirika wa Marekani.

Rais wa Czech Vaclav Klaus amesema wanaona kuwa ni muhimu sana kwa Rais Bush kuahidi kuchukua hatua zote kuelezea mambo hayo kwa Urusi na kwa Rais Putin.

Akiwa mjini Prague Bush amesema makombora hayo ya kujihami barani Ulaya yanakusudia kujilinda dhidi ya vitisho vya mataifa ya kihuni.

Amesema Urusi sio adui yao.Adui wa mataifa huru kama lao watakuwa ni wale wenye misimamo mikali wenye itikadi kali au mataifa ya kihuni yanayojaribu kuushinikiza ulimwengu ulio huru ili kwamba kuendeleza malengo ya itikadi zao.Msimamo wake kwa makombora ya kujihami ni hatua halisi ya kujihami isoilenga Urusi.

Maafisa wa serikali ya Marekani wamekuwa wakirudia kusema mara kwa mara kwamba mpango huo wa makombora ya kujihami ni dhidi tu ya vitisho vya mataifa ya kihuni ikiwemo Iran.

Urusi imekataa kukubali hakikisho hilo la Marekani kwamba makombora hayo yamekusudiwa kujihami na mashambulizi dhidi ya mataifa ya kihuni ili kufuta tuhuma kwamba mataifa ya magharibi yamekuwa yakijilimbikizia silaha za nuklea.

Mbali na kukutana na Putin katika mkutano wa viongozi wa Kundi la Mataifa Manane G8 Bush pia amemualika kiongozi huyo wa Urusi nchini Marekani hapo mwezi ujao.

Bush amesema ujumbe wake kwa Putin katika mikutano hiyo utakuwa huu:

Urusi haipaswi kuhofia makombora hayo ya kujihami na kwa nini isishirikiane na mfumo huo wa makombora kwanini isishiriki na Marekani.Ametaka watume magenerali wao na wanasayansi kuona vipi mfumo huo utafanya kazi na wawe na nafasi ya kujadili suala hili katika kikao cha wazi kabisa.

Mjini Prague mamia ya wananchi wa Zzech wameandamana jana usiku kupinga mipango ya Marekani ya kuweka makombora hayo ya kujihami wakibeba mabango yanayosomeka Aibu kwa Bush hatutaki Kambi na kwamba Makombora hayo yananuka uvundo wa kifo.

 • Tarehe 05.06.2007
 • Mwandishi Mohamed Dahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHD6
 • Tarehe 05.06.2007
 • Mwandishi Mohamed Dahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHD6

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com