1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vipi kuulisha chakula ulimwengu ?

20 Januari 2009

Jibu:Maonesho ya kilimo Berlin

https://p.dw.com/p/GctH

Vipi kuupatia chakula umma wa watu bilioni 9 katika sayari hii ?

Katika maonesho makuu ya kilimo yanayofanyika sasa mjini Berlin,Ujerumani,maarufu kwa jina la "Grune Woche" wiki ya kilimo,chakula na mazao ya kilimo yamesheheni:Kuna milima ya chizi,nyama na matunda na mboga mbali mbali.

Kwa jumla kuna hadi aina 100 za vyakula kutoka kila pembe ya dunia.

Kutokana na makisio ya hivi sasa ya Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) , wanadamu bilioni 1 wanakufa na njaa ulimwenguni.Kifanyike nini kuepusha njaa ? Hii ndio mada inayowaumiza kichwa wakati huu wajumbe kutoka nchi 30 mbali mbali ,miongoni mwao mawaziri wa kilimo kwenye maonesho hayomjini Berlin.

Ukweli unajulikana:Hadi ifikapo 2050 idadi ya wakaazi ulimwenguni itapngezeka kiasi cha mara tatu na kufikia bilioni 9.Lakini katika kima kama hicho,nani atawalisha binadamu ?

Swali hili linahitaji jibu la haraka na katika maonesho ya kilimo ya Berlin-Grune Woche-huko Berlin mabingwa 1000 kati yao mawaziri wa kilimo kutoka nchi 30 mbali mbali wanajadiliana.

Rais wa Shirikisho la wakulima la Ujerumani Gerd Sonnleiter anasema:

" Sawa na mkutano wa Davos nchini Uswisi ulivyo kwa uchumi wa dunia, mji wa Berlin, uwe na utakuwa msukumo kwa juhudi za kupigania dunia isio na dhulma na ya haki.Wanasiasa na wanaviwanda, wapaswa kusaka njia za kufikia ulimwengu wa haki na wa amani na masharti ya kwanza kufikia shabaha hiyo,ni kuhakikisha kuna chakula cha kutosha duniani.Kuwa na haki ya kujipatia chakula."

Hayo anayosema rais huyo wa Shirikisho la wakulima la Ujerumani,Gerd Sonnleietner alilotoa mbele yaukumbi wa majadiliano kama dai lake kuna wenye dhamana kama hiyo miongoni mwa wanasiasa.Hii alibainisha wazi waziri wa kilimo wa Ujerumani mkutanoni Bibi Ilse Aigner:

"Haki ya kujipatia chakula ni haki ya binadamu ambayo lazima itekelezwe.Kila nchi ,iweke usoni kabisa jukumu la kuona wananchi wake wanajipatia chakula cha kutosha na lazima wapatiwe chakula."

Alisema bibi Ilse Aigner.

Lakini, vipi ikiwa nchi fulani haimudu au haitaki kuhakikisha wananchi wake wanapata chakula cha kutosha ?

Katika nchi zinazotawaliwa kidikteta mfano wa Korea ya Kaskazini au Zimbabwe,serikali za huko hazijali sana endapo wananchi wanakufa na njaa.

Vita vya kienyeji,kukandamizwa wananchi n a rushua ni sababu kuu zinazosababisha njaa.Kati ya watu milioni 963 wanaokufa na njaa,zaidi ya nusu ni wakulima pamoja na familia zao.

Mwishoni mwa mwaka uliopita ,hali ilizidi kuwa mbaya kutokana na kupanda kwa bei za vyakula muhimu kama anavyosimulia Bw.Sonnleitner.

Anasema kwamba, mwaka 2008 ni mwaka uliotuamsha sote kwamba, malighafi sio zinapatikana kila wakati na bila kikomo na hazitauzwa kwa bei za chini kama zamani.Shehena za nafaka ulimwenguni zimepungua sana .

Mwaka 2008 ulikuwa mwaka mzuri wa mavuno n a kwa sababu hii pekee bei zipipungua mwishoni mwa mwaka.Mnamo miaka iliopita mahitaji ya chakula mara nyingi yakipindukiwa na pato.Ndio maana bei za nafaka ulimwenguni ziliteremka kuliko wakati wowote miaka ya nyuma .Kimsingi ni muhimu sana kuzalisha zaidi mazao.Lakini hii ni rahisi kusema kuliko kutenda.

Kwa mfano, ardhi ya kulimia anasema mtaalamu wa kikemia Stefan Marcinowski,mjumbe wa bodi ya kiwanda cha kikemia cha BASF alisema, "hatuwezi kupanua mashamba ya klulimia tutakavyo.Tangu 1960 imedhihirika tumebakiwa na nusu tu ya mashamba ya kulimia ili kuwalisha wanadamu.Hali hii itaselelea hivy