Viongozi wa upinzani wanakutana nchini Pakistan | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 07.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Viongozi wa upinzani wanakutana nchini Pakistan

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Bbibi Benazir Bhuto ameanza mazugnumzo na viongozi wengine wa upinzani. Mkutano huo unajadili mbinu za kuigeuza hali ya hatari iliyotangazwa na rais Pervez Musharraf.

Bibi Benazir Bhutto

Bibi Benazir Bhutto

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Bbibi Benazir Bhuto ameanza mazugnumzo na viongozi wengine wa upinzani. Mkutano huo unajadili mbinu za kuigeuza hali ya hatari iliyotangazwa na rais Pervez Musharraf.

Bibi Benazir Bhutto anafanya mazungumuzo na viongozi wenzake wa upinzani ukiwemo muungano wa vyama vya United Council of Action unaovijumuisha vya vya kidini.

Lakini chama cha PML kinacho ongozwa na waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif hakishiriki kwenye mkutano huo.

Akifafanua ni kwa nini amechukua hatua ya kukutana na viongozi wa upinzani badala ya rais Pervez Musharraf ambae ndie aliyekuwa anafanya nae mazungumzo tangu awali bibi Benazir Bhutto amesema, mazungumzo baina yao yamekwama kwa sababu hapo mwanzo walikuwa wanajadili njia za kurejesha demokrasia lakini anasema kinachomshangaza na kumshtua zaidi ni kwamba badada ya kurejea kwenye demokrasia anaona Pakistan imeishia kwenye sheria za kijeshi.

Bibi Bhutto ameongeza kusema kuwa jenerali Musharraf ikiwa kweli anataka kuirejesha demokrasia basi itambidi atangaze kuwa anajiuzulu madaraka ya kijeshi

Bibi Benazir Bhutto ambae chama chake cha PPP kilikuwa kinajitenga na maandamano yaliyoitishwa na mawakili ametangaza kwamba atafanya mkutano mkubwa siku ya ijumaa katika mji wa Rawalpindi.

Meya wa jiji hilo amesema kuwa mkutano huo utavunjwa na wala hautaruhusiwa kufanyika.

Wakati huo huo shinikizo za kidiplomasia dhidi ya kupinga hali ya hatari iliyotangazwa nchini Pakistan na jenerali Musharraf na kumtaka kiongozi huyo arejeshe hali ya kiraia nchini humo zinaendelea kumiminika.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amesisitiza kwamba Pakistan lazima irejee katika demokrasia na utawala wa kiraia.

Bwana Ban Ki Moon amerejelea mwito wake wa kuachiliwa viongozi wa kisiasa na wanasheria waliokamatwa wakati wa vurugu za hivi majuzi.

Katibu mkuu pia ametaka uhuru wa vyombo vya habari urejeshwe.

Lakini balozi wa Pakistan katika umoja wa mataifa Munir Akram amepuuza madai hayo, amesema hayo ni mambo ya ndani ya nchi yake na kwamba umoja wa mataifa hauna haki ya kuingilia kati.

Viongozi wa kimataifa pia wanaendelea kulaani hatua ya rais Pervez Musharraf ya kutangaza hali ya hatari.

Waziri wa mambo ya nje wa Australia Alexander Downer amemtaja jenerali Musharraf kuwa ni dikteta na kumtaka arejeshe demokrasia nchini mwake haraka iwezekanavyo.

Mgombea wa urais nchini Marekani bibi Hilary Rodham Clinton pia amejiunga na viongozi wa Marekani kupinga hali ya hatari iliyotangazwa na rais Pervez Musharraf nchini Pakistan amesema kuwa jenerali Musharraf amefanya kosa kubwa sio tu kwa nchi yake bali hata katika juhudi za kupambana na ugaidi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com