1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa mataifa ya Afrika wakutana Mauritania

Sekione Kitojo
1 Julai 2018

Viongozi wa  Afrika wanakutana Mauritania Jumapili(01.07.2018)katika mkutano wa siku mbili utakaolenga biashara huria, upatikanaji wa fedha, mapambano dhidi ya rushwa pamoja na mizozo mingi  ya kiusalama barani humo.

https://p.dw.com/p/30cIn
Ruanda Kigali Unterzeichnung Afrikanisches Freihandelsabkommen
Picha: Imago/Xinhua/G. Dusabe

Zaidi  ya  viongozi  wa  serikali  na  taifa  40 wanatarajiwa  kuwasili  katika  mji  mkuu  wa Mauritania  , Nouakchott, wakiungana  siku  ya  Jumatatu na  rais  wa  Ufaransa  Emmanuel Macron , ambaye  anatarajiwa  kusukuma juhudi  za  kiusalama  katika  eneo  la  Afrika kaskazini.

Kiongozi  wa  Rwanda  Paul Kagame, ambaye anashikilia  urais wa  kupokezana  wa  Umoja wa  Afrika  ( AU )wenye  wanachama  55, atatoa  rai  kuhimiza  biashara  huru.

Frankreich Präsident Emmanuel Macron & Paul Kagame, Präsident Ruanda
Paul Kagame (kulia) akisalimiana na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa(kushoto)Picha: Getty Images/AFP/L. Marin

Kwa  hivi  sasa, mataifa  ya  Afrika  yanafanya baina  yao  biashara  ya  kiasi  cha  asilimia 16  tu , kiasi  kidogo  cha  biashaa  ya  kimkoa  ikilinganishwa  na   mataifa  ya  America kusini, Asia, Amerika  kaskazini  na  Ulaya.

Lakini   mabadiliko  yako  karibu.

Mwezi  Machi , mataifa  44 yalitia  saini  mkataba  kuunda  eneo  la  biashara  huru  la  bara la  Afrika , African Continental Free Trade Area, (CFTA), unaoonekana  kuwa ni eneo  kubwa kabisa  la  kibiashara  duniani  kwa  mujibu  wa  nchi  zinazoshiriki.

Matunda ya  majadiliano  ya  miaka  miwili, CFTA ni mradi  muhimu  wa  AU kwa  ajili  ya ujumuisho  mkubwa  zaidi  wa  bara  la  Afrika.

Iwapo  mataifa  yote 55 wanachama  hatimaye  yatatia  saini, itaunda  kundi  ambalo linajumla  ya  pato  jumla  la  taifa  GDP linalofikia  dola  trilioni 2.5, na kukusanya  soko  lenye jumla  ya  watu  bilioni  1.2.

Ruanda Kigali Unterzeichnung Afrikanisches Freihandelsabkommen
Viongozi wa mataifa yaliyotia saini mkataba wa ACFTAPicha: Getty Images/AFP/STR

Mapambano dhidi  ya  rushwa

Lakini  mataifa  mawili  yenye  uchumi  mkubwa  katika  bara  hilo, Afrika  kusini  na  Nigeria, ambayo rais  wake, Muhammadu Buhari , anatarajiwa  kufika  katika  mkutano  huo, ni mataifa  ambayo  hayamo  katika  mkataba  wa  CFTA.

Kagame  pia  atasukuma  mbele pendekezo  la  miaka  miwili  sasa  lenye lengo la kuimarisha  mfuko  wa  fedha na  kupunguza  Umoja  wa  Afrika  kutegemea  wafadhili  wa nje, suala  ambalo  mara  nyingi  huzushwa  na  wakosoaji  ambao  wanauona  umoja  huo kuwa  mkubwa  kwa  maneno  lakini  hakuna  vitendo.

Wazo hilo ni  kuhusu  kodi  ya  asilimia  0.2  katika  baadhi  ya bidhaa zinazoingizwa  katika bara  la  Afrika  ili  kuimarisha "Mfuko wa  Amani" kwa  ajili  ya  kugharamia  ujumbe  wa amani  na  usalama.

Ruanda Kigali Unterzeichnung Afrikanisches Freihandelsabkommen
Katibu msaidizi wa Umoja wa Mataifa Vera Songwe akihutubia mkutano wa FTCAPicha: picture-alliance/Xinhua/G. Dusabe

Katika  bajeti  ya  AU  ya  dola  milioni 769, dola  milioni 451 zinatoka  kwa  wafadhili  wa kigeni, ambao  huchangia pia  asilimia  97  ya  mipango  yake.

Kupambana  dhidi  ya  rushwa  ni  lengo  kuu  la  mkutano  huo, wanaopambana  na  rushwa wataangalia  kwa  kina  kile  ambacho  Afrika  inalenga  kufanya  katika  kupunguza  sifa yake  kuwa  ni  eneo  lililochafuka  zaidi  katika  kufanya  biashara duniani.

Shirika  la  Transparent International , katika kielelezo  chake  cha  hivi  karibuni  katika rushwa  kilichochapishwa  mwezi  Februari , imesema  rushwa  imejikita  nchini  Sudan Kusini na  Somalia, miongoni  mwa  mataifa  mengine. Lakini  pia  imesema  picha  ya  jumla  ya bara  la  Afrika  imechanganyika, na  kundi  la  uongozi  linajitokeza  katika  kupambnana  na rushwa,

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe

Mhariri: Zainab Aziz