Viongozi wa kundi la FDLR wakamatwa nchini Ujerumani. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 17.11.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Viongozi wa kundi la FDLR wakamatwa nchini Ujerumani.

Polisi wa Ujerumani wamewatia nguvuni viongozi wawili wa kihutu ambao wameongoza harakati za waasi nchini humo.

Wakishiriki kwa pamoja ujenzi mpya wa nchi yao vijana wa Rwanda Wahutu na Watutsi kutoka katika kundi la vijana la kuondoa mauaji ya kimbari wanafanyakazi kwa pamoja kuhamasisha watu kuishi kwa amani.

Wakishiriki kwa pamoja ujenzi mpya wa nchi yao vijana wa Rwanda Wahutu na Watutsi kutoka katika kundi la vijana la kuondoa mauaji ya kimbari wanafanyakazi kwa pamoja kuhamasisha watu kuishi kwa amani.

Kalsruhe :

Polisi ya Ujerumani imewatia nguvuni viongozi wawili wa Kihutu ambao wameongoza harakati za waasi wanaoendesha visa vya ubakaji, mauaji na uharibifu mashariki mwa Congo.

Dr Ignace M mwenye umri wa miaka 46 ambaye ni rais wa kundi la waasi la FDLR anatakiwa nchini Rwanda kwa uhalifu wa kivita.

Maafisa wa Ujerumani wanalichukulia kundi hilo kuwa la kigaidi.

Mwingine aliyekamatwa ni Naibu wake anayejulikana kwa jina la Straton M mwenye umri wa miaka 48.

Mwendesha mashitaka wa Shirikisho alisema kuna ushahidi wa kutosha kuwa, wanahusika na uhalifu wa kivita.

Huenda wakafunguliwa mashtaka hapa Ujerumani.

 • Tarehe 17.11.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/KZFC
 • Tarehe 17.11.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/KZFC
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com