1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Ni sifa ya aina yake na ya kipekee ulimwenguni kote"

Zainab Aziz Mhariri: Josephat Charo
13 Septemba 2019

Wayahudi na waislamu wanakusudia kuongeza nguvu ya sauti zao katika juhudi za kupambana na ongezeko la siasa kali za mrengo wa kulia barani Ulaya. Viongozi wa dini hizo watakutana siku ya Jumapili nchini Italia.

https://p.dw.com/p/3PYW9
Religion House of One
Picha: Lia Darjes

Viongozi wa dini hizo kutoka nchi 15 watahudhuria mkutano huo siku ya Jumapili kwenye mji  wa Matera kusini mwa Italia ili kujadili namna ya kuimarisha uhusiano wa dini zao. Mhandisi wa mambo ya ujenzi kutoka  mji wa Vienna Austria Tarafa Baghajati ambaye anatambulika kuwa miongoni wa Maimamu mashuhuri barani Ulaya alipozungumza na DW alisema anafikiri kuwa huu ni mkutano wa aina yake duniani. 

Imamu huyo Baghajati alishirikiana na maimamu wengine kuanzisha jumuiya ya umoja wa waislamu wa Austria mnamo mwaka 1999. Na mwaka 2006 jukwaa la pamoja la waislamu na wakristo lilifuatia. Miaka mitatu iliyopita baraza la viongozi wa kiislamu na kiyahudi kwenye taasisi ya Mfalme Abdullah ya mjini Vienna ya kuendeleza mdahalo kati ya dini na tamaduni, KAICIID ilianzishwa. Baada ya mikutano ya mara kwa mara imani iliendelea kujengeka katika jumuiya hiyo.

Religion House of One Pfarrer Gregor Hohberg, Rabbiner Dr. Tovia Ben-Chorin Imam Kadir Sanci
Kushoto: Kasisi Gregor Hohberg, Katikati:Rabai Dr. Tovia Ben-Chorin Kulia: Imam Kadir SanciPicha: Lia Darjes

Hata hivyo pana changamoto. Baraza hilo linafadhiliwa na  Saudi Arabia. Mnamo mwezi juni baraza la kitaifa la Austria lilipiga kura ya kujiondoa kwenye baraza hilo la waislamu na wayahudi. Katika tamko lake baraza hilo la viongozi wa kiislamu na kiyahudi lilielezea masikitiko  yake juu ya hatua hiyo. Mustakabal wa baraza hilo sasa umo mashakani.

Mkutano wa Jumapili wa mjini Materra utawaleta pamoja wajumbe kutoka Ireland, Ugiriki, Lithuania, Ureno na Romania. Masuala yatakayojadiliwa ni pamoja na kusisitiza kwamba dini za kiyahudi na kiislamu ni sehemu ya utamaduni wa Ulaya. Hayo amesema katibu mkuu wa baraza la uongozi la waislamu na wayahudi, Gady Chronich.

Baraza hilo la kidini na kitamaduni limebainisha kampeni iliyoanzishwa hivi karibuni nchini Italia dhidi ya utamaduni ya tohara na uchinjaji halali wa wanyama. Kampeni hiyo inaathiri uhuru wa dini hizo mbili na ndiyo sababu kwenye mkutanao wa mjini Materra, wajumbe wanakusudia kuunda kamati ya kushughulikia suala hilo barani Ulaya kote. Kila upande utawakilishwa na wajumbe wawili kwenye kamati hiyo. Imamu Baghajati ametahadharisha juu ya siasa za mrengo mkali wa kulia barani Ulaya.

Chanzo:Strack Christoph /DW