1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa EU waahidi umoja na mshikamano

25 Machi 2017

Katika azimio la kuadhimisha miaka 60 tokea kuasisiwa kwa Umoja wa Ulaya viongozi wa umoja huo wameahidi kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya umoja huo kwa kuziruhusu nchi kuzidi kuungana kwa kasi tofauti.

https://p.dw.com/p/2ZxAa
EU feiert 60. Geburtstag in Rom
Picha: Reuters/T. Gentile

Azimio hilo lililotolewa Jumamosi (25.3.2017) linakuja wakati Umoja wa Ulaya ukikabiliwa na shinikizo kutokana kuongezeka kwa sera za kizalendo,mzozo wa wakimbizi na kujitowa kwa Uingereza katika umoja huo.

Wakuu wa nchi na wa serikali wameahidi kuufanya Umoja wa Ulaya uwe na nguvu zaidi na imara kwa kupitia umoja mkubwa zaidi na mshikamano miongoni mwa nchi wanachama.Pia wameweka dira kwa Umoja wa Ulaya ambapo kwayo nchi wanachama zinaweza kuamuwa kushirikiana kwa karibu zaidi katika masuala fulani kuziruhusu nchi kadhaa kuchukuwa hatua za kuungana zaidi katika kasi tofauti.

Viongozi hao wameandika "Tutachukuwa hatua kwa pamoja katika kasi tofauti na kuziharakisha pale inapobidi" Wameongeza kusema kwamba wataendelea kuheshimu mikataba ya umoja huo kuweza kuungana na juhudi za ushrikiano wa karibu zaidi baadae.

Azmio halikupita kwa urahisi

Italien EU Gipfel Beata Szydto
Waziri Mkuu wa Poland Beata Szyslo.Picha: picture alliance/AP Photo/A.Tarantino

Hata hivyo kupitishwa kwa azimio hilo hakukuwa rahisi yaani bila ya mvutano.Poland ilitishia kwamba haingelisaini waraka huo kutokana na kupinga kwake kipengee cha kuanzisha kile kinachojulikana kama Ulaya ya mwendo kasi tofauti jambo ambalo kwa hakika litaziacha nyuma baadhi ya nchi.

Lakini baadae usiku hapo Ijumaa Waziri Mkuu wa Poland Beata Szydlo alipoashiria kuwa tayari kwake kupitisha azimio hilo kwa kusema kwamba madai ya Poland yametimizwa kabla ya kuondoka kwenda Rome.Haiko wazi madai gani hayo yaliotimizwa kwani maudhui yake yako kama yalivyo wakati rasimu hiyo ilipokuwa imekamilika hapo Jumatatu.

Wakati wa kusaini azimio hilo Syzdlo alifanya utani

juu ya utata huo wakati alipoishikilia hewani kalamu kwa kusita kusaini azimio hilo kabla ya kufanya hivyo.

Mwelekeo wa pamoja

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ambaye ni mmojawapo wa wale wanaounga mkono wazo la kuendelea kuungana kwa Umoja wa Ulaya kwa kasi tofauti amesema msimamo huo haina maana kuwa ni mwisho wa Umoja wa Ulaya wa kawaida.

Amesema "Tumesema wazi kabisa: Tunataka kusonga mbele kwenye mwelekeo wa pamoja."

Italien EU Gipfel deutsche Kanzlerin Angela Merkel
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.Picha: picture-alliance/AP Photo/A.Tarantino

Merkel ametaja kuendelea kujitolea kwa Umoja wa Ulaya kwa haki za asili na uhuru katika umoja huo kama vile soko la pamoja,nyendo huru za watu,bidhaa,huduma,mtaji na uhuru mwengine wa Ulaya ukiwemo uhuru wa kuzungumza, dini na uhuru wa kuzungumza.Amesema jambo hilo linazidi kuwafanya wawe na nguvu zaidi.

Ugiriki pia ilitishia kuzuwiya kuunga mkono maudhui ya azimio hilo baada ya katafautiana na wakopeshaji wa Umoja wa Ulaya kuhusiana na mashari ya mageuzi kwa nchi hiyo ilioelemewa na madeni makubwa.

Ni baada tu ya Rais wa Halmashauri ya Umoja ya Ulaya Jean -Claude Juncker kuyakinisha uungaji mkono wa Umoja wa Ulaya kwa maendeleo ya kijamii ya Ugiriki kwamba Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras pia amekubali kusaihi waraka huo.Viongozi wamesisitiza kwamba Ugiriki haitoachwa nyuma kwa azimio hilo kutaja kuanzisha kwa "Ulaya ya kijamii" kufanya suala hilo kuwa kipau mbele kwa umoja huo kuendeleza usawa wa kijamii ikiwa ni pamoja na kupunguza kwa ukosefu wa ajira.

Sherehe za kuadhimisha miaka sitini ya kusainiwa kwa Mkataba wa Rome mwaka 1957 ambao hatimae ulipelekea kuundwa kwa Umoja wa Ulaya ziligubikwa na miito kadhaa ya viongozi wa Umoja wa Ulaya kuamsha tena Umoja wa Ulaya.

Mwandishi : Mohamed Dahman/dpa/AP

Mhariri : Suddi Mnette