1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Ouattara vimeingia ikulu kumtoa Laurent Gbagbo

Oumilkher Hamidou6 Aprili 2011

Laurent Gbagbo, hataki kukubali kwamba ameshindwa licha ya kuvunjika serikali yake na jeshi kutangaza kuweka chini silaha katika wakati ambapo vikosi tiifu kwa Alassane Ouattara vimeivamia Ikulu kumtoa kwa nguvu.

https://p.dw.com/p/10oBD
Vikosi tiifu kwa OuattaraPicha: AP

Katika wakati ambapo Ufaransa na Umoja wa mataifa wanashikilia atie saini hati kuhakikisha anayapa kisogo madaraka na kumtambua mpinzani wake kama rais, Gbagbo ameshaonya kamwe hatokubali.

Sitambui ushindi wa Outtara, kwanini mnataka nitie saini hati kama hii?amesema Laurent Gbagbo wakati wa mahojiano ya simu pamoja na kituo cha televisheni cha Ufaransa-LCI.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa, Alain Juppé, anasema, hata hivyo, wanaamini hatimae atatanabahi na kujiepusha na opereshini za kijeshi. Waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa amekosoa kile alichokiita " ukaidi usiokuwa na maana."Gbagbo hana matumaini yoyote,watu wote wamemkimbia" ameshadidia.

Elfenbeinküste Unruhen nach Wahl
Rais anaetambuliwa kimataifa Alassane OuattaraPicha: AP

Hata msemaji wa waziri mkuu wa serikali ya Alassane Ouattara, Sindou Méité, anahisi Laurent Gbagbo hana njia nyengine isipokua kun'gatuka. Akizungumza na Deutsche Welle, Sindou Méité amesema:

"Muda wa Gbagbo umekwisha. Hana tena njia. Kama mnavyojua, majenerali wake wengi, na washauri wake wamekimbilia katika ubalozi wa Ufaransa na kutangaza kuweka chini silaha. Wengi wa wanamgambo wa Gbagbo wametupilia mbali silaha zao. Laurent Gbagbo amejifungia-zama zake zimekwisha- enzi yake imemalizika. Suala kuhusu hatima ya rais huyo wa zamani linajadiliwa hivi sasa."

Hata mkuu wa vikosi vya Ufaransa, amirijeshi Edouard Guillaud amesema "ni suala la masaa tu hadi Laurent Gbagbo atakapo'ngoka na kusisitiza rais huyo anaemaliza wadhifa wake,alikuwa nusra ajiuzulu mara mbili tangu ijumaa iliyopita.

Elfenbeinküste Unruhen Abidjan UN Truppen
Vikosi vya umoja wa mataifa vyapiga doria AbidjanPicha: picture-alliance/landov

Ripoti za hivi punde zinawanukuu mashahidi wakizungumzia juu ya mizinga na risasi zinazofyetuliwa karibu na ikulu ya Gbagbo. Wanamgambo wa Allasane Ouattara wameingia katika eneo hilo,kama wanavyosema "kumtoa kwa nguvu Gbagbo ndani ya handaki alimojificha."

Zaidi ya watu 1500 wameuwawa nchini Côte d'Ivoire tangu November 28 iliyopita, na mahakama ya kimataifa ya uhalifu inazungumza na nchi za Afrika Magharibi ili kukusanya maelezo kuhusu visa vya kikatili vilivyotokea nchini humo.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/afp,reuters

Mhariri: Miraji Othman