1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEritrea

Vikosi vya Eritrea bado vyatekeleza mauaji ya raia wa Tigray

Tatu Karema
2 Desemba 2022

Wanajeshi wa Eritrea wameendelea kuwauwa mamia ya raia katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia na kufanya unyanyasaji mwingine wiki chache baada ya pande mbili zinazozozana kutia saini mkataba wa amani.

https://p.dw.com/p/4KPKT
Sudan Äthiopische Flüchtlinge Tigray Um Raquba
Picha: Hussein Ery/AFP

Kulingana na habari zilizokusanywa kati ya Novemba 17 na 25 na kituo cha dharura cha Tigray, vikosi kutoka nchi jirani ya Eritrea, ambavyo vimepigana pamoja na jeshi la Ethiopia katika mzozo huo uliodumu kwa miaka miwili, vimewaua raia 111 na kuwajeruhi wengine 103 katika eneo la Mashariki mwa Tigray.

Ripoti hiyo pia inasema kwamba kulikuwa na visa 39 vya utekaji nyara na kupotezwa kwa raia kulikofanywa na wanajeshi hao wa Eritrea pamoja na uporaji mkubwa unaojumuisha uharibifu wa nyumba 241.  Mmoja wa raia waliotekwa nyara baadaye alipatikana akiwa ameuawa.