1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikapu kama njia ya maridhiano kati ya raia wa Rwanda

Gregoire Nijimbere20 Oktoba 2006

Nchini Rwanda, wajani wa mauaji ya halaiki na wale wa wahalifu wa kivita, wanashirikiana bega kwa bega katika shughuli za kutengeneza vikapu wanavyouzisha nchi za nje. Hivyo, wameonekana kujijengea njia yao ya maendeleo na maridhiano ya kitaifa wakati mahakama zikijaribu kuleta sheria.

https://p.dw.com/p/CHmH
Mabaki ya wahanga wa mauaji ya kimbali ya 1994 nchini Rwanda
Mabaki ya wahanga wa mauaji ya kimbali ya 1994 nchini RwandaPicha: AP

Kwa muda ma mia ya miaka utengenezaji wa vikapu nchini Rwanda umekuwa ni moja kati ya sanaa za kazi ya mkono na kuwa kazi ya upuuzi kiasi. Kwa sasa, vikapu hivyo vinavyotengenezwa kienyeji vimeanza kuwa kivutio nchini Marekani na kuwajumuisha kwa namna hiyo wahutu na watutsi pamoja wakati bado mahakama zikijaribu kuleta upatanishi kupitia sheria.

Katika maonyesho yaliyofanyika Macy mjini New York nchini Marekani wiki iliopita, wanawake kadhaa kutoka Rwanda walionyesha mtindo mwingine wa vikapu na kudhihirisha uwezo wao wa kiufundi kwa watu waliokuwa wamekuja kushuhudia. Yule aliyewatambulisha wanawake hao wa Rwanda kwenye maonyesho hayo, alikuwa ni Willa Shalit, msaani wa kimarekani na vile vile mfanyabiashara ambae njia hiyo ya amani walioshika raia hao kutoka Rwanda ni kiungo kati ya soko la Macy na watengenezaji.

Alisema ´´ Vikapu hivyo kutoka Rwanda vilikuwa havijauzwa kwa kiwango hiki hapo kabla´´.

Matokeo yake katika sekta ya kiuchumi tayari yamejitokeza nchini Rwanda hususan katika maeneo ya vijijini ambako kuna umaskini. Kiasi cha wanawake 2,500 wamekuwa wakitengeneza vikapu hivyo kama njia ya kusaka amani na kujiendeleza kiuchumi.

Fuko la maendeleo la Umoja wa mataifa kwa ajili ya akinamama ambalo huwasaidia makundi ya wasana hao kwa kuwapa mikopo, linaamini kuwa hilo linasaidia kupunguza kubugdhiwa nyumbani na waume zao kwa sababu wanaweza kugharamia mahitajio yao na wakati mwingine huwashirikisha hata wanamume zao katika kazi hizo.

Hata wale wanaotembea na virusi vya ukimwi, wanaweza kununua madawa na kujipatia lishe bora na hivyo wameanza kuwa na umarufu kijamii.

´´Wakati mwanamama mmarekani ananunua kikapu hiki, huwapatia akinamama hao wa Rwanda chakula, nguo na hivyo wanaishi´´. Alisema Consolate Mukanyiligira wa shirika la Avega la kupambana na mauaji ya kuangamiza halaiki ya watu.

Viongozi wa makundi hayo ya akinama kutoka Rwanda yanayyohusika na shughuli za utengenezaji vikapu hivyo, wanasaka maendeleo ya kiuchumi na pia njia ya maridhiano. Kwani wanashirikiana pamoja wahutu na watutsi. Kila mmoja humfunza mwingine kwani kazi isiofanywa na mtu moja, alielezea bibi Marie Claudine Mukamabano.

Kwa hiyo kazi hiyo ya sanaa imeanza kufanikiwa pale mahakama za Rwanda bado zimekuwa zikijaribu kuleta maridhiano ya taifa kupitia sheria. Lakini hadi sasa, kiasi ya wafungwa 120,000 wanasubiri kukatiwa kesi katika jela mbali mbali nchini rwanda.

Mahakama za kijadi za Rwanda maarufu ´´Gacaca´´, mpaka sasa zimekuwa zikijaribu kurejesha mwafaka kati ya raia lakini baadhi ya mashirika ya kutetea haki za binaadamu yanazilaumu kuwa wakati mwingine hutoa hukumu bila ushahidi na baadhi ya majaji walihusika katika maujaji ya kimbali ya mwaka wa 1994. Na isitoshi, daima kulingana na mashirika hayo ya kutetea haki za binaadamu, mahakama hizo hushughulikia mara nyingi katika sehemu za mijini na kuziacha sehemu za vijijini.

Shirika la akinamama hao wanaotengeneza vikapu´´ Dufutanye ´´ maana yake tushirikiane kwa pamoja ambalo limeundwa kwa ushirikiano na wahutu na watutsi ni mfano kwa jamii ya Rwanda ya nje na ndani ya nchi.