Vijana wa Mashariki ya Ujerumani miaka 20 baada ya muungano | Muungano wa Ujerumani | DW | 03.10.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Muungano wa Ujerumani

Vijana wa Mashariki ya Ujerumani miaka 20 baada ya muungano

Vijana wa Ujerumani ya mashariki hawaoni tofauti kati yao na wenzao wa Ujerumani magharibi. Kwa hiyo wanakulia katika Ujerumani tofauti kabisa. Wengi wangependa kuhamia katika shule za upande wa Ujerumani magharibi.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Karl-Liebknecht, mjini Frankfurt Oder

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Karl-Liebknecht, mjini Frankfurt Oder

Tarehe 3 mwezi wa Oktoba mwaka huu yaani Jumapili ijayo, Ujerumani itaadhimisha miaka 20 ya Muungano kati ya Mashariki na Magharibi. Jee hali ikoje katika maisha ya vijana hivi sasa. Vijana kutoka eneo la Ujerumani ya mashariki hawaoni tofauti kati yao na wenzao wa eneo la Ujerumani magharibi. Kwa hiyo wanakulia katika Ujerumani tofauti kabisa. Wengi wangependa kuhamia katika shule za upande wa Ujerumani magharibi. Sekione Kitojo anawasimulia zaidi.

Frankfurt an der Oder: Kwa Wajerumani ya mashariki wengi zaidi si jambo linalowezekana, kwa upande wa kijiografia. Mji huo uko mkabala na mpaka na Poland. Kwa wengi wa watu wa Ujerumani ya magharibi hii ina maana ya kuongezeka kwa watu wasio na ajira na kuporomoka kwa mambo. Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Karl-Liebknecht wanakerwa na dhana kama hiyo. Kwa kuwa mtu yeyote anayeripoti kuhusu sisi, anazungumzia tu kuhusu ukosefu wa ajira ama watu wenye msimamo mkali, anasema Florian Hundertmark mwenye umri wa miaka 17. Kwa hiyo mtu hawezi kuwaona kwa mtazamo mzuri , watu wa magharibi kutoka Frankfurt.

Florian anaishi na Käthe mwenye umri wa miaka 18 na Jörn , mwenye umri wa miaka 16 katika kitongoji cha Oder. Vijana hao wanasoma katika madarasa ya juu katika shule hiyo ya sekondari. Upande wa pili nchini Poland , kuna mji wa Slubice, si mbali sana na inaweza kusikika kengele ya kanisa la Maria. Kwa kweli hapa mtu anaweza kufanya kila kitu anachopenda. Ni mahali pazuri sana , anasema Jörn. Lakini watu wanahamia sehemu nyingine.

Wakati vijana kutoka Frankfurt an der Oder wakikumbuka kuhusu muungano wa nchi mbili za Ujerumani, kuhusu Ujerumani magharibi, haliji suala la kisiasa ama historia. Linakuja suala hali yao ya baadaye katika soko la kazi. Kiwango cha ukosefu wa ajira katika Ujerumani mashariki unafikia asilimia 11.5, ambapo ni karibu mara mbili kuliko Ujerumani ya magharibi. Mwaka 1990 mjini Frankfurt kulikuwa na watu 88,000. Miaka 20 baadaye mabadiliko yamesababisha watu karibu 30,000 kuuhama mji huo. Hata Käthe, Jörn na Florian wanataka kuhamia katika majimbo mengine ya Ujerumani. Florian anataka kusomea kuhusu utengenezaji wa magari, mafunzo hayo yanapatikana tu upande wa magharibi, anasema. Ndio sababu ningependa sana kubakia katika maeneo haya ya karibuni.

Miaka 20 baada ya muungano kumekuwa na tofauti ya kiuchumi kati ya vijana wa mashariki na magharibi. Vinginevyo wanakubaliana vijana hao wote, kwamba Ujerumani haikugawika, anahisi Jörn. Mtu anasikia kila mara kuhusu ukuta, lakini nafikiri , taratibu hilo linaondoka. Wanafunzi hao wa madarasa ya juu wanaifahamu Ujerumani kuwa ni nchi tu iliyoungana. Wamezaliwa kati mwaka 1992 na 1994.

Kundi la muziki maarufu walipendalo, kilabu ya michezo, likizo katika eneo la Mallorca, ni masuala ya kitamaduni yanayowashughulisha vijana hawa, ambao kiuhalisi wamekua kama vijana wa Ujerumani. Anaona hivyo pia Thomas kutoka katika taasisi ya utafiti ya TNS Infratest.

Ukilinganisha kizazi cha watu wa mashariki na magharibi , unaweza kusema kundi hili la vijana ndio la kweli, anasema Gensicke. Mtafiti huyo alizaliwa katika mji wa Magdenburg upande wa mashariki na akahamia Ujerumani ya magharibi baada ya muungano. Historia yake inamfanya kuwa katika nafasi ya kutazamwa katika masuala aliyosomea ya sayansi.

Kwa hali yoyote ile, kuna tofauti, anasema Gensicke. Vijana katika Ujerumani mashariki wanautilia shaka mfumo wa kisiasa. Wakati tunapowauliza vijana , iwapo wanaona demokrasia inafanyakazi vizuri, utawaona vijana wengi wa mashariki wakitoa hoja za umuhimu wa kufanyia mageuzi. Kuhusiana na hilo wanamaana hata upande wa Ujerumani magharibi. Na hali hii ni mpya pia kwa upande wa mashariki.

Je mtazamo huu wa ukosoaji unaleta changamoto kwa nchi nzima? Hapana, wanasema wanafunzi hao la shule ya sekondari ya Liebknecht. Tumeridhika, kwamba kuna umoja, anasema Inka Sörries wa kidato cha 12. Katika upande wa mashariki kuna uhuru ambao unamipaka mingi, kwa mfano marufuku ya kusafiri nje.

Ossis, Wessis, ikiwa na maana wamashariki na wamagharibi, maneno haya yanajitokeza kila mara. Na ni kwasababu yanatumiwa kama maneno tu ya utani kwa vijana wa shule, ambao wamehamia baada ya muungamo na wazazi wao mjini Frankfurt. Miaka miwili nyuma walikutana nchini Ufaransa na vijana wawili kutoka katika majimbo ya Bayern na Hessen, anasema Käthe. Walikuwa wanafahamu mjini wa Frankfurt/Oder uko wapi.

 • Tarehe 03.10.2010
 • Mwandishi Benjamin Hammer
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PRzc
 • Tarehe 03.10.2010
 • Mwandishi Benjamin Hammer
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PRzc
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com