1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo kutokana na virusi vya corona duniani vyafikia 60,000

Sekione Kitojo
5 Aprili 2020

Rais wa Marekani Donald Trump amewaonya wamarekani kujitayarisha  kwa  idadi ya kutisha  ya  vifo vinavyotokana  na  virusi  vya  corona katika  siku  zijazo wakati  idadi  jumla ya  vifo  duniani  kote ikifikia 60,000.

https://p.dw.com/p/3aTBo
Coronavirus Ecuador Guayaquil Angehörige fordern Herausgabe von Toten vor Krankenhaus
Picha: AFP/E. Ortiz

Kesi zilizothibitishwa  na  wagonjwa wa  virusi  vya  COVID-19 nchini  Marekani  jana Jumamosi (04.04.2020) imepindukia  watu 300,000, lakini  Ulaya  inaendelea  kuadhibiwa na janga  hilo ambalo limesababisha  karibu nusu ya watu wote  duniani  kote  kujifungia ndani  ya  majumba yao kwa  gharama  kubwa ya  uchumi  wa  dunia.

Deutschland Krankenhausärzte erhalten Anweisungen zu einem Beatmungsgerät am Universitätsspital Eppendorf in Hamburg
Wagonjwa mahututi nchini Marekani waongezeka kutokana na virusi vya coronaPicha: picture-alliance/AP Photo/A. Heimken

Zaidi ya  vifo  vya  watu 45,000 duniani  kote  vimetokea  katika  mataifa  ya  Ulaya, ambapo Uingereza  imeripoti kiwango  cha juu  kipya cha  vifo  kwa  siku, na  kufikisha idadi  jumla  ya vifo  kuwa  4,300 kutoka  jumla  ya  kesi za  maambukizi 42,000.

Malkia Elizabeth wa pili atatoa  hotuba  maalum ya binafsi  leo Jumapili (05.04.2020) kuwataka  watu  kusimama  na  kupambana  na changamoto  hii  inayotokana  na  virusi  vya corona, na  binafsi  kuwashuruku wafanyakazi  wanaowahudumia  wagonjwa  wa  COVID-19.

Großbritannien London Queen Elizabeth II und Prince Philip Trooping the Colour
malkia Elizabeth atalihutubia taifa la Uingereza Picha: picture-alliance/abaca/T. Akmen

"Nina  matumaini  katika  miaka  inayokuja  kila  mmoja  ataweza  kujivunia  ni  kwa  njia  gani aliweza  kupambana  na  changamoto hii," atasema  katika  hotuba  hiyo, kwa  mujibu wa vipande  vilivyotolewa  jana  Jumamosi.

Kwa hivi  sasa  kuna  zaidi  ya  kesi milioni 1.2 zilizothibitishwa  za  mambukizi  ya  virusi  vya corona  duniani  kote, na  kiasi  ya  watu 65,000  wamefariki  tangu  virusi  hivyo  vilipozuka nchini  China  mwishoni  mwa  mwaka  jana, kwa  mujibu wa  idadi  iliyojumlishwa  na chuo kikuu  cha  Johns Hopkins.

USA Schutzmasken in einem Geschäft in Kalifornien
Vifaa vya kujikinga na maradhi ya COVID-19 vilivyopelekwa jimboni Califonia nchini MarekaniPicha: picture-alliance/NurPhoto/Y. Cao

Trump  amesema  Marekani  inaingia  katika "wakati  ambao ni wa hali  ya kutisha" kwa "idadi  mbaya kabisa."

"Hii  huenda  itakuwa  wiki  ngumu  kabisa," alisema  katika  Ikulu  ya  White House. "kutakuwa  na  vifo  vingi sana."

Wakati  huo  huo , rais  huyo  amesisitiza  kuwa  Marekani  haiwezi  kuendelea  kufungwa kwa milele.

"Mapambano dhidi  ya  virusi  ni  muhimu, lakini hatuwezi  kuiharibu  nchi  yetu," amesema. "Nilisema  tangu  mwanzo , tiba haiwezi  kuwa  mbaya  kuliko  matatizo."

USA Präsident Donald Trump Coronavirus Pressekonferenz
Rais wa Marekani ameonya Wamarekani "kutarajia wiki ngumu". Picha: Getty Images/W. McNamee

Kitisho cha  mikusanyiko  mikubwa  kimeonekana  tena  mwishoni  mwa  juma  hili, mara  hii nchini  Pakistan ambako maafisa  wanajaribu  kuwafuatilia  na  kuwaweka  katika  karantini mamia  kwa  maelfu  waumini  ambao  walihudhuria  tukio  kubwa  la  Kiislamu  mwezi uliopita.

Zaidi ya watu 150  ambao wamehudhuria  wamethibitishwa  kuambukizwa  na  virusi  vya corona hadi sasa, na watu wawili  wamekufa. Wageni  kutoka  nchi  kadhaa  pia  walikwenda katika  tukio  hilo, ambalo lilifanyika   licha  ya  serikali  kuomba  kufutwa  kutokana  na  kitisho cha  virusi.