1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifijo na nderemo Kenya baada ya kuapishwa Rais Barack Obama

Thelma Mwadzaya21 Januari 2009

Nchini Kenya shangwe , vifijo na hoi hoi vilitawala nchi nyote baada ya kuapishwa rasmi kwa Rais wa Marekani Barack Obama.

https://p.dw.com/p/GdU0
Rais Barack Obama akila kiapoPicha: AP

Raia wa Kenya waliserebuka kila mahali kadhalika balozi nchini humo ziliandaa karamu maalum.Magazeti nchini Kenya nayo pia yalimpongeza Barack Obama katika tukio hilo la kihistoria.Itakumbukwa kuwa babake Barack Obama anatoka Kenya.Mwandishi wetu wa Nairobi,Kenya Alfred Kiti ana taarifa zaidi.