VIENNA:Ban Kim Moon atilia mashaka mkataba wa NPT | Habari za Ulimwengu | DW | 01.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VIENNA:Ban Kim Moon atilia mashaka mkataba wa NPT

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban-Ki-Moon ameonya kwamba mkataba wa kuzuia uenezaji wa sialaha za Nuklia unakabiliwa na mzozo kufuatia kuongezeka kwa mvutano juu ya mpango wa Nuklia wa Iran.

Ban Ki Moon aliyasema hayo katika ujumbe wake wa kufungua mkutano wa wiki mbili kuhusu mkataba huo wa NPT mjini Vienna.

Mkutano huo unahudhuriwa na mataifa 188.

Jaribio la bomu lililofanywa na Korea Kaskazini mwaka jana pamoja na juhudi za Iran za kurutubisha madini ya Uranium na kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa kumeuweka pabaya mkataba huo wa kuzuia uenejazi wa sialaha za Nuklia.

Ujerumani ambayo ni mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya imesema uzuiaji wa kueneza sialaha za Nuklia na kukongoa sialaha hizo ni mambo ya lazima kwa ajili ya amani ya kimataifa na usalama.

Ujerumani ikizungumza kwa niaba ya umoja huo pia imeikosoa Iran na kuitaja kuwa ni kitisho kwa mkataba wa NPT
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com