Vienna. Shirika la Atomic halifahamu iwapo Iran inataka bomu la kinuklia. | Habari za Ulimwengu | DW | 05.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Vienna. Shirika la Atomic halifahamu iwapo Iran inataka bomu la kinuklia.

Kiongozi mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la nishati ya Atomic , Mohammed El Baradei, amesema kuwa shirika lake bado haliwezi kutathmini iwapo Iran inataka kuwa na silaha za kinuklia.

Katika mkutano wa bodi ya magavana wa shirika hilo la IAEA mjini Vienna , El Baradei amesema kuwa baada ya uchunguzi wa muda wa miaka minne , shirika hilo limefikia hali ya mkwamo.

Ameongeza kuwa anaimani kuwa suluhisho kuhusiana na suala la kinyuklia la Iran linaweza tu kufikiwa kupitia majadiliano.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com