VIENNA: Kurt Waldheim amefariki akiwa na miaka 88 | Habari za Ulimwengu | DW | 15.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VIENNA: Kurt Waldheim amefariki akiwa na miaka 88

Kurt Waldheim aliekuwa rais wa zamani wa Austria na pia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amefariki Vienna akiwa na umri wa miaka 88.Waldheim alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa awamu mbili na kama rais wa Austria kuanzia mwaka 1986 hadi 1992.Kipindi chake kama rais wa Austria kiligubikwa na habari zilizofichuliwa kuwa alikuwepo katika kikosi cha jeshi la Ujerumani ambacho kilifanya ukatili katika Balkan wakati wa Vita Vikuu vya Pili.Austria ilitengwa na jumuiya ya kimataifa kwa sababu Waldheim alikataa kuzungumza kuhusu maisha yake wakati wa kipindi hicho cha Nazi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com