1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Bernard Kouchner akosolewa

17 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOx

Waziri wa mambo ya nje wa Austria bibi Ursula Plassnik amemkosoa waziri mwenzake wa Ufaransa Bernard Kouchner kuhusu kuutahadharisha ulimwengu juu ya vita dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran.

Bibi Ursula amesisitiza kuendeleza majadiliano na nchi hiyo.

Wakati huo huo shirika la kimataifa linalosimamia matumizi ya nyuklia linapanga kukutana na nchi wanachama 144 wa baraza la usalama la umoja wa mataifa katika mji wa Vienna huku Iran ikiwa ndio ajenda kuu ya mkutano huo.

Mkuu wa maswala ya atomiki wa Iran Reza Aghazadeh ameuambia mkutano wa shirika la kimataifa linalosimamia nyuklia la IAEA kwamba nchi za magharibi zinapendelea njia za makabiliano badala ya majadliano dhidi ya taifa huru la Iran.

Msimamizi mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la IAEA bwana Mohamed El Baradei amekosoa miito ya kuivamia Iran, ameeleza kwamba hatua ya aina hiyo inafaa tu kuchukuliwa iwapo hakuna njia nyingine yoyote.