VICENZA:Waandamanaji wapinga upanuzi wa kituo cha Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 17.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VICENZA:Waandamanaji wapinga upanuzi wa kituo cha Marekani

Maelfu ya watu wamemiminika katika mji wa Vicenza kaskazini mwa Italia kupinga mpango wa kutaka kupanua kituo cha kijeshi cha Marekani.Ulinzi umeimarishwa karibu na kituo hicho cha kijeshi, maafisa wakiwa na hofu kuwa wafuasi wa misimamo mikali huenda wakajipenyeza na kusababisha ghasia.Serikali ya Marekani inataka kuwahamisha wanajeshi wake waliopo Ujerumani hivi sasa,ambao ni kama 2,000 na kuwapeleka Italia.Kwa hivyo, idadi ya wanajeshi wa Kimarekani katika kituo cha cha Vicenza itakuwa kama 5,000.Suala hilo limezusha mabishano makali katika serikali ya waziri mkuu wa Italia,Romano Prodi yenye sera za wastani za mrengo wa shoto.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com