Vettel anyakua taji lake la nne la Formula One | Michezo | DW | 29.10.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Vettel anyakua taji lake la nne la Formula One

Baada ya kushindataji la ulimwengu la Formula One kwa mara ya nne mfululizo, changamoto nyingine inayomkabili Sebastian Vettel ni kujaribu kuwavutia mashabiki wa na kuheshimiwa madereva wenzake

Kijana huyo Mjerumani mwenye umri wa miaka 26, kwa mara nyingine tena alitawala kuanzia mwanzo hadi mwisho katika mbio za mkondo wa India hapo jana Jumapili na kuliongeza jina lake katika orodha ya mabingwa wa Formula One Juan Manuel Fangio na Michael Schumacher kama dereva wa tatu tu kushinda mataji manne mfululizo yan ulimwengu. Dereva mwingine pekee kufanya hivyo ni Alain Prost.

Baada ya kumaliza wa kwanza katika mkondo wa jana wa India Grand Prix, ilimbidi atie kidogo mbwembwe katika ushindi wake kwa kufanya mizunguko kadhaa na gari lake huku akitoa wingu kubw ala moshi mweupe kabla ya kuondoka garini mwake, na kuuonesha hesima umati kwa kupiga magoti huku akiinamisha chini kichwa chake. Hata hivyo hatua hiyo ilimsababishia adhabu kwa kutozwa faini pamoja na timu yake ya red Bull ya euro 25,000, kwa kutoelekea moja kwa moja katika sehemu iliyotengwa kumalizia mbio. Hata hivyo adhabu hiyo haijatia doa sherehe za ushindi wake.

Mwandishi. Bruce Amani/AFP/Reuters

Mhariri: Yusuf Saumu