1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Venezuela yatuma wanajeshi eneo la maandamano

Admin.WagnerD21 Februari 2014

Serikali ya Venezuela imeamuru kutumwa wanajeshi katika maeneo ya mji wa mpakani ambao kumekuwa ongezeko la wanafunzi wanaoandamana yalioanza zaidi ya wiki mbili zilizopita

https://p.dw.com/p/1BDEb
Venezuela Studentenproteste in Caracaserhaftung von Leopoldo Lopez
Waandamanaji wakikabiliana na polisi mjini CaracasPicha: Reuters

Amri hiyo inatolewa wakati rais wa taifa hilo Nicolas Maduro akikaidi kwa hasira kabisa wito wa Marekani wa kumtaka azungumze na wanasiasa wa upinzani.

Maandamano yaliyotapakaa nchini nzima, yanayoongozwa na wanafunzi na upinzani yamesababisha vifo vya watu 4 na wengine wengi kujeruhiwa. Ghasia hizo zinaelezwa kuwa ni miongoni mwa changamoto kubwa tangu kiongozi huyo achukue madaraka baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa taifa hilo Hugo Chavez mwaka jana.

Karibu kila siku kumekuwa na maandamano, mikusanyiko na baadhi ya matukio hayo yamesababisha vurugu katika mji mkuu Caracas na miji mingine ambapo wanaoukosoa utawala wa Maduro wanasema yanatokana na kuzorota kwa hali ya uchumi, kuenea kwa wimbi la vitendo vya uhalifu mitaani, rushwa na ugumu wa upatikanaji wa ajira kwa raia wengi wa taifa hilo.

Kutumwa kwa sakari

Serikali yenye kuufata siasa za mrengo wa shoto inayoongozwa na Maduro, imetuma kikosi cha askari wa miamvuli katika mji wa San Cristobal, sehemu ambayo ni kiini cha maandamano hayo yalioanza Februari 4 mwaka huu.

Studenten demonstrieren auf dem Plaza Alfredo Sadel
Waandamanaji wakiwa katika eneo la Alfredo SadelPicha: DW/Oscar Schlenker

Hatua hiyo ya kijeshi inatokana na madai ya serikali kwamba raia wa Colombia wanavuka mpaka kufanya harakati za kijeshi katika ardhi ya Venezuela. Katika maeneo ya mji huo, San Cristobal ambao kumekuwa na mapambano kati ya polisi na waandamanaji karibu kila siku maduka yamefungwa na mitaa imekuwa kimya kabisa.

Mtangazaji wa kituo kimoja cha televisheni katika mji huyo amesema jana usiku kulisikika milio ya risasi, mabomu ya kutoa machozi katika jitihada za polisi za kutawanya waandamanaji. Mkasa huo ulitokea kabla mawasiliano ya internat kukatwa. Mwandhishi habari Beatriz Font aliongoeza kusema mpaka muda huu hawana mawasiliano ya Internet. Na kwamba baadhi ya watu wanakabiliwa na tatizo la maji na umeme.

Wakati huo huo Maduro ametishia kuvuruga matangazo ya kituo hicho cha televisheni kwa kile alichodai ni kuendeza propaganda za Marekani. Amemshabuliwa kwa maneno makali rais Barack Obama, ambae aliitaka serikali ya Venezuela kuwaachia huru waandamanaji waliowekwa kizuizini na kushughulikia kwa kwa dhati kabisa malalamiko ya watu wake. Lakini serikali ya Maduro imekiita kitendo hicho cha Obama ni sawa na kuingilia mambo ya ya ndani ya Venezuela.

Jumapili iliyopita Maduro aliamrisha kufukuzwa nchini humo maafisa watatu wa ubalozi wa Marekani akiwatuhumu kwa kukutana na viongozi wa wanafunzi kupanga njama kwa kisingizio cha kutaka kuwapa viza. Hata hivyo serikali ya Marekani imekanusha madai hayo.

Mwandishi: Sudi Mnette APE
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman