1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Venezuela yarudisha uhusiano na Colombia

10 Machi 2008

Venezuela imesema inapanga kurudisha uhusiano wa kawaida na Colombia ikiwa ni siku chache tu baada ya kusitisha baina ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/DLXi

CARACAS

Wizara ya mambo ya nje mjini Caracas imesema katika taarifa kwamba itaufunguwa tena ubalozi wake mjini Bogota haraka iwezekanavyo. Wanadiplomasia wa Colombia ambao walitimuliwa ana Rais Hugo Chavez pia wataruhusiwa kurudi nchini Venezuela.

Taarifa hiyo imesema kwamba uamuzi huo umekuja baada ya mkutano wa viongozi wa Ijumaa katika Jamhuri ya Dominica ambao umesaidia kutuliza mvutano kati ya Rais Chavez na Rais Alvaro Uribe wa Colombia.

Mgogoro huo umezushwa kutokana na shambulio la wanajeshi wa Colombia la kumvuka mpaka wa Ecuador na kuuwa waasi 20 wa kundi la FARC mwishoni mwa juma.

Uribe aliahidi katika mkutano huo wa viongozi kwamba hakutakuwepo na marudio ya mashambulizi ya kuvuka mpaka.