VATIKAN CITY : Erdogan kukutana na Papa Benedikt | Habari za Ulimwengu | DW | 27.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VATIKAN CITY : Erdogan kukutana na Papa Benedikt

Waziri Mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan amebadili mipango yake na atakutana na Papa Benedikt wa 16 nchini Uturuki hapo kesho.

Kwa mujibu wa makao makuu ya kanisa katoliki Vatikani Erdogan awali alikuwa alipanga asikutane na Papa kutokana na kwenda kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO huko Latvia.

Msemaji wa Vatikani Mchungaji Federico Lombardi amesema leo hii hivi sasa Rais huyo wa Uturuki atakutana na Papa kwenye uwanja wa ndege baada ya kuwasili kwake na kabla ya yeye kuondoka kuelekea Latvia.

Ziara ya Papa Benedikt nchini Uturuki inapingwa vikali na baadhi ya Waturuki waliokasirishwa kutokana na hatuba aliyoitowa papa huyo hapo mwezi wa Septemba ambapo alikariri maudhui ya kale yaliohusisha Uislamu na matumizi ya nguvu.

Maelfu ya Waturuki waliandamana mjini Instanbul hapo jana kupinga ziara hiyo na kumwita Papa Benedict kuwa adui wa Uislamu

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com