VATICAN: Papa Benedikt XVI akutana na Mfalme Abdullah wa Saudia Arabia | Habari za Ulimwengu | DW | 07.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VATICAN: Papa Benedikt XVI akutana na Mfalme Abdullah wa Saudia Arabia

Papa Benedikt XVI na Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia wamekuwa na mkutano wa kihistoria katika Vatican.Viongozi hao wawili walijadili hali ya Wakristo wachache nchini Saudi Arabia ambako huishi kiasi ya Wakatoliki milioni moja.Wakristo nchini Saudi Arabia huruhusiwa kuabudu nyumbani kwao tu.

Wakati wa mkutano huo wa dakika 30,viongozi hao walizungumzia pia mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati uliokwama na haja ya kuwepo ushirikiano zaidi kati ya Wakristo,Waislamu na Wayahudi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com