Van Gaal: nikosoeni mimi, sio wachezaji wangu | Michezo | DW | 06.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Van Gaal: nikosoeni mimi, sio wachezaji wangu

Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amejibu shutuma zinazoendelea kutolewa na wafuasi wa klabu hiyo kwa kuwataka wamkosoe yeye na wala siyo wachezaji wake walio chini ya shinikizo

United wako katikati ya kipindi kigumu ambapo wameshindwa kufunga bao katika michuano minne mfululizo ya kandanda la Uingereza.

United imefunga magoli 15 katika mechi 11 za Ligi ya Premier na watahitaji ushindi dhidi ya West Bromwich Albion hii leo ili kuwawekea mbinyo viongozi Manchester City na Arsenal.

Lakini Van Gaal anasema wafuasi wa Man Utd wanapaswa kukosoa mbinu zake yaani filosofia yake na wala sio wachezaji maana wanafanya mambo kubwa magumu hata zaidi kwao.

Mourinho: wachezaji wangu hawana wasiwasi

Jina lake bado tu linatamba katika vyombo vya habari. Jose Mourinho. Na kocha huyo anasema kukosekana kwake katika uwanja wa Britiannia katika mchuano wa leo dhidi ya Stoke City hakutaiathiri timu yake ya Chelsea wakati ikijaribu kujinyanyua kutokana na matokeo mabaya katika ligi ya Premier.

Mourinho atakosekana kwenye benchi la kiufundi wakati akitumikia adhabu ya kufungiwa nje ya uwanja mchuano mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumtupia maneno makali refa Jon Moss wakati wa kichapo cha The Blues dhidi ya West Ham United. Chelsea kwa sasa wako katika nafasi ya 15.

Jumapili Aston Villa watawaalika Manchester City wakati Arsenal wakikabana koo na Tottenham Hotspurs katika mpambano mtamu wa watani wa tangu jadi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Gakuba Daniel

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com