Uturuki kwenye mkondo unaofaa | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 14.09.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Uturuki kwenye mkondo unaofaa

Ujerumani na Umoja wa Ulaya kwa pamoja zinaiunga mkono Uturuki baada ya matokeo ya kura ya maoni ya katiba kuridhia mabadiliko.

default

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan

Kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle,hatua hiyo ni muhimu kwa Uturuki iiliyo katika harakati za kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya.Kiasi ya asilimia 59 ya wapiga kura waliyaunga mkono mapendekezo ya kuzifanyia mabadiliko ibara 26 za katiba.

Türkischer Premierminister Erdogan mit Ehefrau Emine

Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan na mke wake Emine Erdogan:Bado ana mvuto mkubwa

Mabadiliko hayo yataugeuza mfumo mzima wa sheria nchini Uturuki,kuyapunguza madaraka ya jeshi pamoja na kuzilinda haki za wafanyakazi wa umma,wanawake na makundi ya kidini yaliyo na wafuasi wachache.Kulingana na Waziri Mkuu wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan,mabadiliko hayo yataiimarisha demokrasia nchini humo.Chama chake cha AK kinachoyaunga mkono mageuzi hayo pia kimefurahishwa na matokeo ya kura ya maoni ya katiba.

DW inapendekeza

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com