1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utawala wa Myanmmar washinikizwa zaidi na jumuiya ya kimataifa

31 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/EAGL

YANGOON

Kwa mara nyingine utawala wa kijeshi nchini Myannmar umejikuta chini ya shinikizo la Umoja wa mataifa,jumuiya ya kimataifa na makundi ya kutetea haki za binadamu baada ya serikali hiyo kuwaondoa kwa nguvu kutoka makambini manusura wa kimbunga cha Nargis.Msemaji wa Umoja wa mataifa amesema ni kitendo kisichokubalika kuwarejesha kwa nguvu watu hao majumbani kwao bila ya kupata msaada wowote.Utawala huo wa kijeshi umefahamisha kwamba unachukua hatua hiyo kutokana na hofu kwamba makambi hayo huenda yakawa makaazi ya kudumu kwa wakimbizi hao.Kwa mujibu wa taarifa za shirika la misaada la UNICEF kiasi makambi manane yamefungwa.Mashirika ya misaada yanasema utawala huo wa kijeshi unaendelea kuzuia juhudi zao za kuwafikia manusura walioko kwenye maeneo yaliyoharibiwa vibaya na kimbunga hicho ya Irrawady Delta.Shirika la msalaba mwekundu linasema wafanyikazi wake wengi bado wanasubiri kupata hati za usafiri licha ya utawala huo wa kijeshi kuahidi kwamba itaruhusu wafanyikazi wote wa kimataifa kuingia nchini humo.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amekosoa hatua ya utawala huo ya kuchelewesha kuruhusu misaada ya kigeni.Amesema ndege za Marekani pamoja na meli zimekwama zikisubiri idhini ya kuruhusiwa kupakua misaada itakayoweza kuokoa maisha ya maelfu ya watu.