1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Utawala wa kijeshi wa Niger wasema upo tayari kwa mazungumzo

16 Agosti 2023

Utawala wa kijeshi nchini Niger umesema jana kwamba uko tayari kwa mazungumzo ya kusuluhisha mzozo uliosababishwa na mapinduzi ya kijeshi mwezi uliopita, wakati Marekani na Urusi zikitoa miito ya suluhu ya amani.

https://p.dw.com/p/4VE3C
Msemaji wa jeshi la mapinduzi la Niger Kanali Amadou Abdramane
Msemaji wa jeshi la mapinduzi la Niger Kanali Amadou AbdramanePicha: ORTN via Reuters

Waziri mkuu mpya Ali Mahamane Lamine Zeine, ameonya baada ya ziara yake nchini Chad kwamba uingiliaji wowote wa kijeshi utasababisha hali mbaya zaidi katika eneo tete la Sahel linalopambana na ugaidi.

Amesema tayari wameonyesha nia ya mazungumzo ya pande zote, ingawa wanasisitiza taifa hilo kuwa huru katika kipindi hiki cha mpito.

Huku haya yakiendelea, wakuu wa majeshi wa Jumuiya ya Maendeleo huko Afrika Magharibi, ECOWAS wanajiandaa kukutana Alhamisi na Ijumaa kuangazia uwezekano wa kuivamia kijeshi Niger.