Uswisi yazuia mali za Ben Ali | Matukio ya Kisiasa | DW | 20.01.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Uswisi yazuia mali za Ben Ali

Serikali ya Shirikisho la Uswisi imezuia mali za rais aliyeondolewa madarakani nchini Tunisia, Zine El Abidine Ben Ali na familia yake zilizoko nchini Uswisi.

default

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uswisi, Micheline Calmy-Rey

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uswisi, Micheline Calmy-Rey amesema anataka kuzuia matumizi yoyote mabaya ya fedha za umma.

Wakati huo huo, Benki Kuu ya Tunisia imeichukua taasisi ya kifedha iliyokuwa inadhibitiwa na mkwe wa Ben Ali.

Mapema, viongozi wa Tunisia walisema pia watachunguza mali za Ben Ali zilizopo nje ya nchi zikiwemo akaunti za benki na nyumba.

Zine El Abidine Ben Ali

Rais aliyeondolewa madarakani Tunisia, Zine El Abidine Ben Ali

Imeripotiwa kuwa Ben Ali aliyekimbilia Saudi Arabia Ijumaa iliyopita aliondoka nchini Tunisia na tani 1.5 za madini ya dhahabu.

Kwa upande mwingine, karibu waandamanaji 2,000 katika mji mkuu wa Tunis wanadai kufukuzwa kwa mawaziri wote ambao wanahusishwa na Ben Ali katika serikali mpya ya muungano.

Na taarifa nyingine zinaeleza kuwa viongozi wa serikali hiyo ya mpito wamewaachilia huru wafungwa wa mwisho wa kisiasa.

 • Tarehe 20.01.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/zzrG
 • Tarehe 20.01.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/zzrG

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com