1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usuluhishi wa Zimbabwe wapiga hatua nzuri

23 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CS9U

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini hapo jana ametangaza kwamba mazungumzo kati ya chama tawala cha ZANU-PF cha Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na chama cha upinzani cha kutetea demokrasia cha MDC yamepiga hatua nzuri sana ya maendeleo.

Mbeki ambaye ameteuliwa hapo mwezi wa Machi na Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC kusuluhisha mzozo wa kisiasa nchini Zimbabwe alikuwa akizungumza kufuatia mkutano wake wa kwanza na Rais Mugabe na viongozi wa MDC tokea kuanza kwa juhudi hizo.

Mbeki amesema amekuwa na mikutano tafauti ya dakika 40 na Mugabe na viongozi wa MDC ambao hawakuweza kutambulika mara moja.