1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usuhuba wa Korea Kaskazini na Afrika haufi leo wala kesho

Saumu Mwasimba
11 Desemba 2017

Wachambuzi wanaofahamu zaidi juu ya usuhuba huo wanaamini Afrika itaendelea kushirikiana na Korea Kaskazini ikiwa si kwa dhahiri basi kwa siri uhusiano huo si rahisi kuvunjika

https://p.dw.com/p/2pA8o
Nordkorea  Kim Jong Un
Picha: picture alliance/dpa/AP Photo/Korean Central News Agency

Ushirikiano wa muda mrefu kati ya Korea Kaskazini na nchi nyingi za Kiafrika ulioanza tangu wakati wa vita baridi hauwezi kumalizika kirahisi. Wakati vikwazo vya  Marekani na Umoja wa Mataifa ukizilazimisha serikali nyingi katika bara hilo la Afrika kujitenga na utawala wa mjini Pyongyang ,uhusiano  wa tangu jadi kati ya nchi hizo na taifa hilo bado haujafutika. Kwa wanaoufuatilia utawala wa Kim Jong Un uwepo wa nchi yake katika bara hilo la Afrika haujatoweka na kwahakika taifa hilo linaendelea kunufaika katika uhusiano huo wa siri  lakini ambao pia ni muhimu kabisa.

Sanamu pamoja makasri yaliyojengwa kwa miuondo ya  kizamani yanaonekana kuwa na thamani kubwa  yaliyotengezwa na wasanii wa Korea Kaskazini yamekuwa yakionekana katika miji mingi ya barani Afrika kuanzia Dakar Senegal,Windhoek Namibia,Maputo Msumbiji ,Harare Zimbabwe hadi Kinshasa katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo. Lakini ushirikiano kati ya utawala wa Korea Kaskazini na serikali za kiafrika unakwenda mbali zaidi ya miradi ya ujenzi.

Wataalamu wanakadiria kwamba ushirikiano wa kiuchumi kati ya Afrika na Jamhuri ya umma wa watu wa Korea Kaskazini unathamani ya kiasi dolla millioni 200 kwa mwaka. Biashara iliyoko juu kabisa kati ya pande hizo mbili zinahusu madini na uvuvi zikifuatiwa kwa karibu na uzalishaji wa silaha wenye utata wa nchi hiyo ya Korea Kaskazini. Licha ya vikwazo vilivyopitishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2006 dhidi ya taifa hilo kama hatua ya kuijibu kutokana na mpango wake wa silaha za nyuklia,ushirikiano wa kijeshi kati ya taifa hilo na washirika wake katika bara la Afrika umekuwa imara zaidi.

Bildergalerie Jahresrückblick 2017 International
Picha: Reuters/KCNA

Mchambuzi kutoka kituo cha wasomi kuhusu masuala ya kimataifa cha Chatham House mjini London Graham Neville anasema nchi kadhaa zinaoneskana kuendeleza ushirikiano wa karibu na Jamhuri hiyo ya watu wa Korea Kaskazini.Zaidi na nusu ya nchi za Kiafrika kiasi nchi 30 zinashirikiana na Korea Kaskazini kwa mtindo wa kuendesha biashara. Biashara ya silaha ambayo imepigwa marufuku kabisa kwa kupitia vikwazo  imezusha wasiwasi katika Jumuiya ya Kimataifa.

 Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamezituhumu nchi 11 za kiafrika kwamba zinajaribu  kutafuta ushirikiano  wa karibu wa kijeshi na utawala wa Kim Jong Un katika ripoti ya Umoja huo iliyochapishwa mnamo mwezi Septemba mwaka huu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo Korea Kaskazini imekubali kusambaza silaha ndogo ndogo katika nchi za Eritrea na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,sambamba na kupeleka makombora ya angani nchini Msumbiji  huku makombora ya kisasa au mifumo ya Radar  ikipelekwa nchini Tanzania. Juu ya Hilo Korea Kaskazini pia imeridhia kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama nchini Angola na Uganfa.

Mwandishi wa ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa  aliyahpoji makampuni mawili ya Korea Kaskazini ambayo yanafanya shughuli zake nyingi Namibia,Makampuni hayo ni Manusudae Overseas Project na Komid ambayo yalijenga makao makuu mapya ya shirika la ujasusi la Namibia mjini Windhoek pamoja na viwanda vya silaha. Ushirikiano huu wa Korea Kaskazini na nchi za Kiafrika haupaswi hata hivyo kuonekana wa kushangaza.

Nafasi ya Korea Kaskazini-Afrika

Uganda EU AMISOM Friedenstruppe
Picha: DW/E. Lubega

Tangu vita vya ukombozi wa bara hilo ,Korea Kaskazini iliamua kujitumbukiza katika usuhuba mkubwa na tawala za kimaxist katika bara hilo. Na wakati wa vita baridi nchi hiyo ilipata sifa kubwa katika bara hilo kwa kuwapa mafunzo muhimu ya kijeshi vikosi vya kiafrika anasema Samuel Ramani,mtaalam kutoka chuo kikuu cha Oxford,kuhusu nchi hiyo iliyotengwa na ulimwengu. Hata hivyo vitendo vya uchokozi vya Kim Jong Un vya kuendeleza majaribio ya makombora na Nyuklia hatimae vimezishawishi nchi kadha za Afrika kurudi nyuma.

Sudan imekata ushirikiano na nchi hiyo,huku Uganda ikiwatimua washauri wa kijeshi wa nchi hiyo ya  Korea Kaskazini na kuahidi pia kuvitekeleza vikwazo vilivyowekwa dhidi ya nchi hiyo.Hivi karibuni pia waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga alitamka wazi kwamba  nchi yake imepunguza kwa kiasi kikubwa ushirikiano wa kidiplomasia na taifa hilo. Namibia kwa upande wake pia imeahidi kufuta mikataba yote iliyosaini na makampuni ya Korea Kaskazini. Huku hatua za kufukuza wafanyakazi 150 kutoka Pyongyang zikichukuliwa na Angola. Lakini juu ya yote msomi kutoka Jumba la Chatham, Neville anasema kutoshiriki Korea Kaskazini katika historia ya ukoloni barani Afrika pamoja na Azma ya nchi hiyo ya kusimama dhidi ya kile inachokiita Nchi za ``Magharibi za ukandamizaji'' hapana shaka kunaifanya nchi hiyo kupendwa na baadhi ya serikali za Afrika.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman