Usugu wa dawa watishio kuongeza vifo
17 Septemba 2024Utafiti kuhusiana na usugu wa dawa hizo, umekadiria kwamba watu milioni 1.91 wanaweza kufa kutokana na changamoto hiyo ifikapo mwaka 2050, ikiwa ni ongezeko la asilimia 70 kwa mwaka, ikilinganishwa na mwaka 2022.
Zaidi ya watu milioni 1 walikufa kutokana na usugu wa dawa kote ulimwenguni kila mwaka, kuanzia mwaka 1990 hadi 2021.
Wataalamu wa kimataifa wanasema wakati ni sasa wa kuchukua hatua za kulinda watu kote ulimwengu kutokana na kitisho kinacholetwa na usugu wa dawa zinazotumika kutibu maambukizi.
Ongezeko hilo huenda likaongeza shinikizo kwenye mifumo ya afya na uchumi wa mataifa pamoja na kuchangia upotevu wa pato la taifa kwa mwaka la kati ya dola trilioni moja hadi 3.4 ifikapo 2030.
Ripoti hiyo ya timu ya kimataifa ya watafiti imo kwenye jarida la tiba la The Lancet.