1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushirika wa Kiuchumi kati ya Afrika na Ulaya ni mbolea ya ukuajii wa uchumi?

Mohamed Dahman27 Aprili 2007

Wajumbe wa Afrika na Ulaya katika mazungumzo juu ya makubaliano ya ushirika wa kiuchumi EPA kwa nchi za mashariki na kusini mwa Afrika wamekanusha shutuma kutoka mashirika ya kiraia ya kienyeji na ya kimataifa juu ya uwezekano wa kuwepo kwa taathira mbaya kutokana na mapendekezo ya makubaliano hayo.

https://p.dw.com/p/CHl5
Ukumbi wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia hapa ndipo yalipo makao makuu ya Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika.
Ukumbi wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia hapa ndipo yalipo makao makuu ya Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika.Picha: picture-alliance/ dpa

Serikali ya Malwi iliandaa mazungumzo ya kiufundi wiki hii kwa nchi 16 zinazohusika na kundi la EPA la nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.Majadiliano hayo yamefanyika huku kukiwa na upinzani kutoka mashirika matano yasio ya kiserikali juu ya taathira mbaya za makubaliano ya ushirika wa kiuchumi kati ya Afrika na Ulaya EPA.

Mashirika hayo yanadai kwamba EPA yumkini ikaharibu uwezo wa Malawi wa kutanuwa uchumi wake katika nyanja mbali mbali na kujenga sekta ya uzalishaji viwandani na mapato kutokana na ushuru pia yatakuwa yamepotea.Umoja wa Ulaya hivi sasa inaujadili mpango huo wa EPA na makundi sita ya nchi za Afrika, Carribean na Pasifiki (ACP).Mpango huo wa EPA unatazamiwa kuchukuwa nafasi ya makubaliano ya zamani ya upendeleo wa biashara yalioanzia miaka ya 1970 na kuendelea.

Alessandro Mariani balozi wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya na mkuu wa ujumbe kwa mkutano wa Malawi anasema wakati wanafikiri hoja na hofu za mashirika hayo yasio ya kiserikali sio za haki wanatakiwa kizishughulikia na kufanya jitihada za kuelezea wananchi kwa jumla kile wanachokifanya na ni nini malengo yao.

Pia amesema hana haja ya kumshawishi yoyote yule juu ya umuhimu wa EPA na faida zake kwa uchumi wa eneo hilo.Hoja ya Mariani ni kwamba watu wanaelewa juu ya yale yanayoweza kufanywa na EPA kadhalika changamoto zake na ugumu wa mazungumzo hayo.

Anautetea Umoja wa Ulaya kwamba hautafuti biashara huru na nchi za Afrika Caribbean na Pasifiki ACP wakati makubalaiano hayo yatapakokuwa yamesainiwa au baada ya hapo na kwamba Umoja wa Ulaya utafunguwa masoko yake kwa wasafirishajii bidhaa nje wa nchi za ACP.

Kwa upande wa serikali ya Malawi katibu wa bishara na maendeleo ya sekta binafsi Newby Kumwembe ana matumaini juu ya makubaliano hayo mapya ya biashara na anayaunga mkono.

Kwa mujibu ya Kumwembe Malawi itatumia fursa ya makaubaliano hayo mapya kushinikiza msaada wa Umoja wa Ulaya katika kuboresha miundo mbinu ya nchi hiyo katika afani kama vile za uchukuzi na nishati.

Mwakilishi wa Malawi katika Shirika la Biashara Duniani WTO Dickson Yeboah anashikilia kauli kwamba nchi zikiwa wanachama wa WTO zina udau katika mfumo wa biashara wa kimataifa na zinaweza kuushawishi mfumo huo.Anaona mfumo wa biashara ya kimataifa unaofanya kazi ipasavyo utaziwezesha serikali kuyaweka wazi masoko yao na kuregeza zaidi mashaarti ya biashara kwa mujibu wa mahaitaji ya biashara,fefdha na maendeleo.

Hata hiyvo waziri wa biashara wa Malawi Ken Lipenga ameelezea wasi wasi wake juu ya umahiri wa wajumbe wa Afrika katika mazungumzo ya kibiashara wakilinganishwa na wenzao wa Ulaya.

Mazungumzo ya biashara hufanyika miongoni mwa nchi zilizoteuliwa kwenye vikao vya faragha vya WTO marafiki wa mwenyekiti wa mikutano hiyo huchaguliwa kukutana tafauti na hata mikutano midogo ya ngazi ya mawaziri huwa ni matukio maalum.

Wajumbe wa EPA wanataka Umoja wa Ulaya usaidie kujenga uwezo wa nchi za kimaskini katika kutekeleza na kufaidika kutokana na kuregezwa kwa masharti ya biashara na ongezeko la kupatikana kwa nafasi za masoko ili kuzisaidia kujumuika kwenye uchumi wa dunia.