1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yadai imedhibiti jaribio la kushambuliwa manuari yake

10 Julai 2024

Shirika la Usalama la Urusi FSB limesema hii leo limetibua njama iliyoitaja kuwa "ya kigaidi" ya kuishambulia meli yake moja ya kivita na kwamba limemkamta shushushu mmoja wa Ukraine aliyehusika na mpango huo.

https://p.dw.com/p/4i6Pq
Meli ya kivita ya Urusi Caesar Kunikov
Meli ya kivita ya Urusi 'Caesar Kunikov', ikifanya safari zake huko Istanbul, Uturuki,Picha: Sedat Suna/epa/dpa/picture alliance

FSB imesema mpango huo uliukuwa unailenga Manuari yake pekee ya kijeshi ya Kuz-netsov ambayo imetia nanga kwenye bandari ya Murmansk kwa ajili ya matengenezo. Taarifa hizo zimetolewa wakati vikosi vya Moscow vimeendelea kuishambulia miji ya Ukraine usiku wa kuamkia leo ikiilenga miundombinu muhimu ya uchukuzi.Kwenye mkoa wa kusini wa Odessa, mashambulizi ya Urusi yaliipiga bandari na kusababisha mauaji ya watu wawili ikiwemo dereva wa Lori la mizigo. Haya yameelezwa na gavana wa mkoa huo Oleg Kiper. Mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 62 ameuwawa kutokana na shambulizi la Urusi kwenye mji wa Nikopol