Urusi na Marekani zabadilishana majasusi | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 09.07.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Urusi na Marekani zabadilishana majasusi

Wizara ya sheria ya Marekani imesema itawarudisha kwao majasusi 10 Warusi kwa mabadilishano na watu wanne wanaozuiliwa nchini Urusi.

Mikhail Semenko anayetuhumiwa kuwa jasusi wa Urusi ambaye amekamatwa Marekani

Mikhail Semenko anayetuhumiwa kuwa jasusi wa Urusi ambaye amekamatwa Marekani

Tangazo hilo limetolewa muda mfupi baada ya majasusi hao 10 kukiri kuwa na hatia mjini New York Marekani kwa makosa madogo ya kuwa mawakala wa serikali ya kigeni bila kibali.

Katika hatua inayohusiana na kesi hiyo, rais wa Urusi, Dmitry Medvedev amewasamehe majasusi wanne walioshtakiwa kwa kutoa habari za siri kwa nchi za magharibi.

Washukiwa hao walitakiwa na serikali ya Urusi kusaini taarifa kukubali makosa yao kama sharti la kuachiwa kwao. Makubaliano ya kubadilishana majasusi hao kati ya Marekani na Urusi yamefikiwa kwa haraka kuliko ilivyotarajiwa.

Mwandishi:Josephat Charo

Mhariri:Aboubakary Liongo

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com