Urusi itaendelea kupeta ? Czech katika mbinyo | Michezo | DW | 12.06.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Urusi itaendelea kupeta ? Czech katika mbinyo

Fainali za kuwania kombe la mataifa ya Ulaya, Uefa , Euro 2012 zinaingia katika mzunguko wake wa pili katika kundi A. Poland na Urusi na Czech na Ugiriki.

Russia's national team pose for a photo prior an international friendly soccer match, against Greece, at Karaiskaki stadium, Piraeus, near Athens, on Friday, Nov. 11, 2011. The draw for the final tournament of the Euro 2012 is to be held on Friday, Dec. 2, 2011 in Kiev, Ukraine. (Foto:Petros Giannakouris/AP/dapd)

Kikosi cha timu ya taifa ya Urusi

Poland inakabiliwa na mtihani mkubwa baada ya mchezo wa kwanza dhidi ya Ugiriki kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Kushindwa dhidi ya Urusi , ambayo imeichapa jamhuri ya Czech mabao 4-1 katika mchezo wa kwanza inaweza kufikisha mwisho ndoto ya Poland katika mashindano haya makubwa ambayo ni mwenyeji mwenza pamoja na Ukraine.

Hatuna hofu , amesema nahodha Jakub Kuba Blaszcykowski wa mabingwa wa Ujerumani, Borussia Dortmund, tunataka kupiga hatua. Katika pambano litakalofanyika mjini Warsaw, linaweza kumuweka katika kurunzi mchezaji mwenzake wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski, ambaye aliweka wavuni goli la Poland dhidi ya Ugiriki siku ya ufunguzi wa mashindano haya ya Uefa , Euro 2012.

Source News Feed: EMEA Picture Service ,Germany Picture Service Poland's Maciej Rybus and Robert Lewandowski (C) celebrate as Greece's Kostas Chalkias lies on the ground, after scoring a goal during their Group A Euro 2012 soccer match at the National stadium in Warsaw June 8, 2012. REUTERS/Pascal Lauener (POLAND - Tags: SPORT SOCCER)

Mshambuliaji Robert Lewandowski.

Goli hilo lilizusha uvumi kama moto katika manyasi wakati wa kiangazi kuwa Manchester United inataka sasa kufunga kibwebwe kumnyakua mshambuliaji huyo hatari wa Dortmund. Kocha Smuda, hata hivyo, amelazimika kumkosa mlinda mlango Wojciech Szczesny wa Arsenal London , baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu na badala yake kumtegemea mlinda mlango namba mbili, Przemyslaw Tyton, ambaye katika pambano dhidi ya Ugiriki alipangua penalti.

Mbinyo kwa Urusi

Kocha Dick Advocaat wa Urusi ameonya, hata hivyo, kuwa kutakuwa na mbinyo wa kufanya vizuri zaidi , baada ya ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya jamhuri ya Czech, na kwamba Urusi inatajwa sasa kuwa moja ya timu zinazoweza kutoroka na kombe hilo.

Russia's head coach Dick Advocaat watches his team during a training session at the Luzhniki stadium in Moscow, Russia, Monday, Oct. 10, 2011. Russia will play their Euro 2012 qualifying soccer match against Andorra on Tuesday. (ddp images/AP Photo/Ivan Sekretarev)

Kocha wa timu ya taifa ya Urusi Mholanzi Dick Advocaat

Kwa ushindi dhidi ya Poland katika mchezo wa pili , Warusi wanaweza kuwa timu ya kwanza kukata tikiti katika duru ijayo ya robo fainali katika michuano hii.

Matatizo ya majeruhi katika kikosi cha Mholanzi Dick Advocaat hakuna, kwa hiyo kikosi cha kwanza kilichoingia uwanjani dhidi ya Jamhuri ya Czech kitaranda tena uwanjani dhidi ya Poland. Tatizo huenda likawa katika upande wa mashabiki wa Urusi. Shirikisho la soka la Ulaya , Uefa, linajadili hatua za kinidhamu dhidi ya chama cha kandanda cha Urusi . Kuna madai ya ubaguzi, mabango yenye matusi pamoja na ufyatuaji wa fataki uwanjani wakati wa mchezo dhidi ya jamhuri ya Czech. Kuna shutuma za kibaguzi, ambazo zinachunguzwa na shirikisho hilo , katika mchezo kati ya Italia na Uhispania pia.

Nani atafunga virago?

Kila timu hapa inataka kusonga mbele, kwa hiyo kila mchezo utakuwa kama fainali.

Ugiriki inaingia uwanjani dhidi ya jamhuri ya Czech. Kocha Fernando Santos anaingia uwanjani akikiongoza kikosi cha Ugiriki kwa mara ya pili katika fainali hizi za kombe la mataifa ya Ulaya, katika mchezo wa kwanza jioni ya leo.

Greece's head coach Fernando Santos from Portugal watches the friendly soccer match between Greece and Romania in Altach, Austria, Tuesday Nov. 15, 2011. (AP Photo/Kerstin Joensson)

Kocha wa timu ya taifa ya Ugiriki Fernando Santos

Kocha Santos, raia wa Ureno, anakabiliwa na upungufu wa wachezaji watatu, Bremmer Sokratis aliyepewa kadi nyekundu, Avraam Papadopoulos, aliyeumia mguu na pia Georgios Fotakis ambaye ana maumivu ya paja.

Jamhuri ya Czech baada ya kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya Urusi ni lazima ishinde iwapo inataka kubakia katika kinyang'anyiro hiki, la sivyo ikipata kipigo tena leo, itakuwa kimsingi imeyapa mkono wa kwaheri mashindano haya.

Mwandishi : Boettcher, Arnulf / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Othman Miraji