1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani: Katumbi aruhusiwe kushiriki uchaguzi DRC

13 Agosti 2018

Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC, wanaendesha juhudi za kidiplomasia kwa ajili ya kuweko na uchaguzi wa amani nchini Congo.

https://p.dw.com/p/334Hp
Moise Katumbi kongolesischer Oppositionsführer
Picha: picture-alliance/Keystone/M. Trezzini

Haya ni baada ya rais Kabila kufahamisha nia yake ya kutowania muhula wa tatu. Wakati huo huo Upinzani umeomba mwanasiasa Moise Katumbi aruhusiwe kurudi nyumbani ilikushiriki katika uchaguzi huo.

Mkutano maalumu wa kujadili  hali ya kisiasa nchini Kongo na Sudan Kusini unatarajiwa hapo kesho mjini Luanda, Angola ambako marais wa kanda ya maziwa makuu na wale wa afrika ya kati watahuzuruia.Lengo la mkutano huo alielezea waziri wa angola wa mamabo ya nje kwamba ni kutaka kuweko na uchaguzi wa amani nchini Kongo.

Rais Kabila amepongezwa kwa kutangaza kuwa hatowania tena urais

Juhudi hizo za viongozi wa kikanda zimedhihirishwa pia na ziara aliyoifanya mwishoni mwa wiki rais wa Afrika ya Kusini,Cyril Ramaphosa ambae pia ni mwenye kit iwa jumuiya ya SADC. Kwenye taarifa yao ya pamoja hapa mjini Kinshasa,Marais Ramaphosa na Joseph Kabila alipongeza hatua iliofikiwa na tume ya uchaguzi katika kukamilisha zoezi la kurejesha fomu kwa wagombea wa kiti cha urais.

DRC Präsident Joseph Kabila
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Joseph KabilaPicha: Reuters/K.Katombe

Kwenye taarifa yao ya pamoja mabalozi wa muungano wa Ulaya,Marekani,Canada, Uswisi na Umoja wa Afrika nchini Kongo walipongeza hatua ya rais kabila ya kuteuwa mgombea mwengine wa chama tawala kwenye uchaguzi wa rais huku wakisisitizia kushirikishwa kwa pande zote kwenye uchaguzi. Msimamo huo ni ule wa kanisa katoliki.

Maaskofu wa Kongo ambao walisuluhisha mazungumz bain aya chama tawala na upinzani mwaka 2016,mawamepongeza hatua ya rais kabila huku wakielezea umuhimu wa kushirikishwa kwa wapinzani wote kwenye uchaguzi.Padre Andre Masinganda ni naibu katibu mkuu wa kongamano la maaskofu wa Kongo

Kutoshirikishwa kwa Katumbi kwenye uchaguzi ujao kutakuwa na vinyume vingi amesema Pierre Lumbi

Wakati hayo yakijiri Mshauri wa zamani wa maswala ya kiusalama wa rais Kabila, Pierre Lumbi ambae hivi sasa anamuunga mkono mpinzani Moise Katumbi amesema kwamba utaratibu wa uchaguzi pasina Moise Katumbi hauaminiki. Kwenye barua ya wazi,Pierre Lumbi amemtolea mwito rais kabila kurahisisha kurejea kwa Moise Katumbi iliashiriki kwenye uchaguzi huo.

Demokratische Republik Kongo Wahlmaschine
DRC itafanya uchaguzi wake Desemba 23Picha: Getty Images/AFP/J. Wessels

Kutoshirikishwa kwa Katumbi kwenye uchaguzi ujao kutakuwa na vinyume vingi amesema Pierre Lumbi. Miongoni mwa masharti ya upinzani kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi ni pamoja na kutokueko na uchaguzi wa mfumo wa komptuta. Kanisa katoliki limeomba kuweko na maridhiano baina ya wanasiasa kabla ya matumizi ya kompyuta kwenye uchaguzi. Padre Masingenda wa CENCO.

Mnamo Agosti 24,tume ya uchaguzi itatangaza daftari la dharura la wagombea wa  kiti cha urais na bunge,kabla ya daftari la  kudumu tarehe 19 Septemba.

Mwandishi: Saleh Mwanamilongo

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman