Upinzani washinda uchaguzi wa rais Paraguay | Habari za Ulimwengu | DW | 21.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Upinzani washinda uchaguzi wa rais Paraguay

-

ASUNCION

Mgombea wa urais wa chama tawala nchini Paraguay amekuabalia kushindwa katika matokeo ya uchaguzi wa rais ambayo yanaonyesha kwamba mgombea wa upinzani ambaye alikuwa askofu Fernando Lugo amepata ushindi mdogo.Matokeo ya mwanzo yameonyesha kwamba Lugo anaongoza kwa asilimia tisa dhidi ya mgombea wa chama tawala Balnca Ovelar.Kwa mujibu wa mahakama ya uchaguzi nchini Paraguay matokeo hayo yametokana na hesabu ya zaidi ya nusu ya vituo vya kupigia kura.Lugo ni mgombea wa chama cha muungano cha mrengo wa kushoto cha Patriotic Alliance for Change na katika kampeini zake ameahidi kulitatua suala linalohusu usawa pamoja na kupambana na rushwa nchini Paraguay.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com