1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani wamuunga mkono El Baradei

Sekione Kitojo30 Januari 2011

Upinzani nchini Misri umekubali kumuunga mkono kiongozi wa upinzani Mohammed El Baradei kuongoza ujumbe wa majadiliano na serikali

https://p.dw.com/p/107VJ
Kiongozi wa upinzani nchini Misri Mohamed El BaradeiPicha: picture-alliance/dpa

Upinzani nchini Misri umesema umekubaliana kumuunga mkono kiongozi wa upinzani Mohamed El Baradei kuongoza ujumbe wa majadiliano kati yao na serikali.

Muungano wa vyama kwa ajili ya kuleta mabadiliko nchini humo, ambao unajumuisha vyama mbalimbali vya upinzani, ikiwemo kile kilichopigwa marufuku cha Udugu wa kiislamu -Muslim Brotherhood-, vimempendekeza bwana El Baradei, ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel.

Ägypten Kairo Proteste
Waandamanaji mjini CairoPicha: picture-alliance/dpa

Wakati upinzani ukiamua hivyo, ghasia nchini Misri zimeiingia siku yake ya sita leo nchini Misri, ambapo waandamanaji wamekusanyika katika eneo la Tahrir mjini Cairo, kumtaka Rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak kuondoka madarakani.

Awali, Rais Mubarak alifanya mazungumzo na Makamu wa rais Omar Suleiman, ambaye alimteua jana kushika wadhfa huo, kwa kile kilichoonekana kuwa ni uwezekano wa kuunda serikali ya mpito.

Ägypten Proteste Chaos
Rais Mubarak akiwa na makamu wa rais Omar Suleiman,(kati)Picha: dapd

Alifanya mazungumzo pia, na maafisa waandamizi wa jeshi la nchi hiyo.

Ulinzi umeimarishwa katika eneo hilo, ambapo helikopta za kivita zilionekana zikipiga doria.

Jeshi la nchi hiyo limewaonya raia kutii amri iliyowekwa ya kutotembea ovyo.

Wakati huohuo nchi kadhaa, zimeanza kufanya mipango ya kuwaondoa raia wake nchini humo.