1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani wamtaka rais Kibaki ajiuzulu

6 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Ckw1

Upinzani nchini Kenya unamtaka rais Mwai Kibaki ajiuzulu kabla kukubali kushiriki kwenye mazungumzo yatakayolenga kuumaliza mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Upinzani umekataa kubadili msimamo wake licha ya rais Mwai Kibaki kusema yuko tayari kuunda serikali ya umoja wa taifa katika juhudi za kumaliza machafuko yaliyotokea nchini Kenya kufuatia kutangazwa kwake kama mshindi wa uchaguzi uliofanyika nchini humo mnamo tarehe 27 mwezi uliopita.

Rais Kibaki alitoa tangazo hilo baada ya kukutana na naibu waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Jendayi Frazer, mjini Nairobi.

Jendayi Frazer alikutana pia na kiongozi wa upinzani bwana Raila Odinga, ambaye amesisitiza rais Kibaki ajiuzulu kwanza kabla kufanyika mashauriano ya kuutanzua mgogoro mbaya zaidi wa kisiasa kuwahi kutokea nchini Kenya katika kipindi cha miaka 25.

Jendayi Frazer atakutana tena leo na viongozi wa kisiasa nchini Kenya.