1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Venezuela unajiandaa kwa maandamano

Oumilkheir Hamidou
4 Machi 2019

Wafuasi wa upande wa upinzani nchini Venezuela wanapanga kuteremka majiani leo baada ya kiongozi wao Juan Guaido kuwataka waandamane dhidi ya rais Nicolas Maduro.

https://p.dw.com/p/3EP2a
Venezuela Cucuta - Unruhen an der Grenze zwischen Kolumbien und Venezuela
Picha: Reuters/M. Bello

Guaido mwenyewe  anajiandaa kurejea nyumbani baada ya ziara ya wiki moja katika nchi shirika za Latin America.

Changamoto kubwa atakumbana nayo Nicolas Maduro pindi Guaido akirejea Venezuela; atalazimika kuamua  ama kumkamata kwa kukiuka marufuku ya kusafiri na kwa namna hiyo kuzusha lawama za walimwengu au kumuachia arejee bila ya pingamizi na kubainisha utawala wake hauna nguvu.

"Nimeamua kurejea nchini. Nnawatolea wito wananchi wa Venezuela wakusanyike katika kila pembe nchi kesho saa tano mchana" amesema Guaido kuoitia mtandao wa kijamii wa twitter.

Baadae alitahadharisha kupitia kanda ya video na akusema "Serikali ikithubutu kuniteka nyara,itakuwa inafanya mojawapo ya makosa yake ya mwisho, na bila ya shaka itafanya kosa hilo wakati huu tulio nao."

Guaido ana nguvu kiasi gani?

Brasilien Treffen Jair Bolsonaro und Juan Guaido in Brasilia
Picha: Agência Brasil/A. Cruz

Guaido anaetambuliwa na zaidi ya nchi 50 kama rais wa mpito wa Venezuela hakusema anapanga kurejea vipi nyumbani ingawa uvumi umeenea atasafiri kwa ndege kutoka mji mkuu wa Colombia Bogota hadi Caracas.

Kuna wanaosema pia huenda akarejea kama alivyotoka Venezuela, kwa kuvuka mpaka wa Colombia alidain wakati ule amesaidiwa na wanajeshi wa serikali ya Maduro.

Guaido alikuwa na mazungumzo pamoja na rais Lenin Moreno katika mji wa mwambao wa Salinas jumamosi iliyopita na baadae kukukutana na wakimbizi wa Venezuela. Ameondoka Salinas  jana mchana bila ya kusema anaelekea wapi.

Brasilien Treffen Jair Bolsonaro und Juan Guaido in Brasilia
Picha: Agência Brasil/A. Cruz

"Guaido anabidi arejee nyumbani na kuendelea kushinikiza akiwa ndani nchini kwakuwa shinikizo la kimataifa bado ni kubwa" amesema Eufracio Infante,sambae ni wakili na mwalimu wa ahistoria nchini Venezuela."Tunakabiliana na hali ngumu na kila dakika inayotujongeza mbele tunataraji haitosababisha balaa" amesema.

Maduro anaeungwa mkono wa jeshi, ambalo ni taasisi yenye nguvu kupita kiasi nchini humo, anajivunia pia uungaji mkono wa Urusi inayokosoa sera za kujiingiza kati Washington  na China inayopigania hatima ya mabilioni ya dola walizoikopesha seerikali ya maduro.

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/AFP

Mhariri: Mohammed Khelef