1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Uganda wapinga mashtaka ya mauaji dhidi ya wabunge

8 Septemba 2021

Upinzani nchini Uganda umetaja hatua ya kuwafungulia mashtaka ya mauaji wabunge wawili wa chama cha NUP kuwa hila za kisiasa ambazo lengo lake ni kujenga hisia hasi za chuki dhidi ya chama hicho. Wabunge hao walisimama kizimbani jana Jumanne na kusomewa mashtaka ya kupanga na kuendesha mauji ya raia wasio na hatia katika kanda ya Masaka kusini mwa nchi. Msikilize Emmanuel Lubega kutoka Kampala.

https://p.dw.com/p/404nL