1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Rwanda wataka msaada kutoka Marekani na Umoja wa Ulaya

Josephat Nyiro Charo7 Juni 2010

Viongozi wa upinzani wanadai serikali ya Rwanda imewabana mno kiasi cha kutoweza kupumua katika ulingo wa kisiasa ili kuweza kumwaga sera zao nchini humo.

https://p.dw.com/p/Nk6S
Rais wa Rwanda, Paul KagamePicha: DW-TV

Vyama vitatu vya upinzani nchini Rwanda vimeiomba Marekani, Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuingilia kati na kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kufungua milango ya ushindani wa kisiasa kuviwezesha vyama hivyo kushiriki katika uchaguzi wa Rais utakaofanyika tarehe 9 mwezi Agosti mwaka huu.

Katika barua iliyotumwa kwa pande hizo tatu, vyama hivyo, Democratic Green Party, PS Imberakuri na FDU Inkingi, vimeeleza kuwa licha ya juhudi zote za kisheria kutaka kushiriki katika uchaguzi huo, hadi sasa serikali imeviwekea aidha kwa kuvinyima usajili, ama kuweka vizingiti vingine vinavyokwamisha shughuli zao. Mwandishi wetu wa mjini Kigali, Daniel Gakuba ametutumia ripoti ifuatayo.

Mwandishi, Daniel Gakuba

Mpitiaji, Peter Moss

Mhariri, Josephat Charo