United kidedea, Arsenal hoi | Michezo | DW | 30.11.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

United kidedea, Arsenal hoi

Manchester United walionyesha cheche zao baada ya kutoka chini magoli mawili walipokwaana na Southampton na kutoa ushindi wa 3-2 huku mshambuliaji kutoka Uruguay Edinson Cavani akicheka na wavu mara mbili.

 

Arsenal walikuwa nyumbani Emirates wakiwaalika Wolverhampton Wanderers na wakabebeshwa magoli mawili kwa moja katika mechi ambayo mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez alipata jeraha baya la kichwa alipogongwa na beki wa Arsenal David Luiz walipokuwa wakiwania mpira wa kona. Ripoti zinaarifu kwamba kwa sasa Jimenez anaendelea vyema ingawa bado yuko hospitali.

Dabi ya London kati ya Tottenham Hotspur na Chelsea iliyompatanisha kocha na mwanafunzi wake, Jose Mourinho na Frank Lampard, iliishia sare ya kutofungana.