1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNICEF yaonya juu ya kizazi kilichopotea kutokana na corona

19 Novemba 2020

Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limeonya juu ya kile linachosema ni "kizazi kilichopotea", katika wakati ambapo virusi vya corona vikiendelea kuathiri elimu, lishe na afya za watoto ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/3lXWU
Symbolbilder | Laut UNICEF können Hunderte Millionen Kinder in Schulen nicht Händewaschen
Picha: picture-alliance/dpa/XinHua/S. Zounyekpe

Katika ripoti yake mpya iliyotolewa leo, UNICEF imegunduwa kwamba watoto na vijana ni asimilia 11 ya watu walioambukizwa virusi vya corona duniani.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, Henrietta Fore, amesema madai ya muda mrefu kwamba ni shida sana kwa watoto kuathiriwa na virusi hivyo  yamethibitika kwamba si kweli.

Ripoti hiyo imebaini kwamba huduma za afya zimeshuka mara tatu kwenye mataifa 140 yaliyofanyiwa uchunguzi kutokana na hofu ya maambukizo.

Takribani watoto milioni 265 duniani kote wanakosa chakula wanachopatiwa wakiwa skuli, ambapo inahofiwa kuwa asilimia 14 kati yao watapata magonjwa yanayohusiana na ukosefu wa lishe bora mwaka huu pekee, hasa kwenye mataifa ya Afrika iliyo kusini mwa jangwa la Sahara na ya Asia Kusini.