1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

UNHCR:Watu 200,000 kutoka Sudan wamekimbilia nchi jirani

12 Mei 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wakimbizi, UNHCR limesema takriban watu 200,000 wameikimbia Sudan na kuingia nchi jirani tangu vilipozuka vita mwezi uliopita.

https://p.dw.com/p/4RHe8
Sudan EU richtet humanitäre Luftbrücke in den Sudan ein
Picha: Amanuel Sileshi/AFP

Watu hao wakiwemo watoto wengi wenye utapia mlo wamewasili nchini Chad. Msemaji wa UNHCR Olga Sarrado ameuambia mkutano wa waandishi habari mjini Geneva kwamba takriban watu 60,000 wamewasili Chad kupitia jangwani ikiwa ni pamoja na watu kiasi 30,000 waliofika siku chache zilizopita.

Soma zaidi:Licha ya makubaliano ya kuheshimu huduma za kibinaadamu, mapigano yaendelea Sudan

Kiasi asilimia 90 ya wakimbizi wapya waliowasili ni wanawake na humusi moja ya watoto wadogo wako kwenye hali ya utapiamlo. Shirika hilo limetowa mwito wa kupatiwa msaada wa haraka wa kifedha kuepusha janga la kibinadamu na kuzuia hali ya wasiwasi.