1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yatoa wito kwa makampuni kutoa fedha ili kuziokoa bahari

28 Juni 2022

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa serikali na makampuni mbalimbali kujiunga na mapambano ya kuziokoa bahari duniani. Guterres anataka ujengwe mfumo endelevu wa kiuchumi kusimamia bahari.

https://p.dw.com/p/4DLWT
2022 UN-Ozeankonferenz
Picha: Carlos Costa/AFP

Takriban watu 7,000 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano unaohusu bahari,ulioandaliwa na  Umoja wa mataifa,huko mji wa Lisbon nchini Ureno. Mkutano huo utahusisha  wakuu wa nchi, wanasayansi na mashirika yasiyo ya kiserikali, ili kutathmini maendeleo katika kutekeleza agizo la kulinda maisha ya majini.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumzia hali iliyopo sasa kuhusu bahari duniani amesema "inasikitisha, tunaiona bahari ni kitu cha kawaida, na leo tunakabiliana na kile ninachoweza kukiita "dharura ya bahari".

Soma pia: Mkutano wa kilele wa kunusuru bahari wafanyika Ufaransa

"Ni lazima tuibadilishe hali hiyo. Ongezeko la joto duniani linasababisha viwango vya joto baharini kuongezeka kwa kiasi kikubwa na kusababisha dhoruba za mara kwa mara. Vina vya maji ya bahari vinaongezeka. Mataifa ya visiwa yanakabiliwa na mafuriko  kama ilivyo pia kwa miji mikubwa ya pwani duniani.'' 

2022 UN-Ozeankonferenz
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres, rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa bahari wa UN uliofanyika mjini Lisbon, Ureno, Juni 27, 2022.Picha: Carlos Costa/AFP

Guterres aliongezea kuwa, kunahitajika biashara ya mfano, ambayo itasaidia bahari kuzalisha chakula na nishati mbadala."Hiyo inahitaji  viwango vipya vya ufadhili wa muda mrefu,"

Taka za plastiki, kikwazo kwa viumbe wa majini

Bahari ni  karibu asilimia 70  ya uso wa sayari, ambapo inazalisha asilimia  50 ya oksijeni na kunyonya asilimia 25 ya kaboni dioksidi

Lakini mabadiliko ya hali ya hewa yanapelekea joto la bahari kufika kiwango cha juu na kutengeneza tindikali zaidi. Aliongezea kuwa tani milioni nane za taka za plastiki huingia baharini kila mwaka."Bila hatua kali, taka za plastiki zinaweza kuzidi samaki wote samaki baharini ifikapo mwaka 2050,"

Mnamo mwezi  Machi, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zilishindwa kukubaliana juu ya mkataba wa kulinda bahari kuu dhidi ya unyonyaji.

Soma pia: Dalili njema zaibuka kwenye mkutano wa Mazingira wa Durban

Peter Thomson, Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya   bahari, aliambia shirika la habari la Reuters kuwa, alikuwa na imani kwamba makubaliano yatafikiwa mwaka huu.

BdTD Portugal | Ocean Rebellion Protest in Lissabon
Mwanaharakati wa shirika la Ocean Rebellion akitembea kushiriki maandamano nje ya mkutano wa bahari wa UN, dhidi ya kile wanachokieleza kama "vita dhidi ya samaki", mjini Lisbon, Juni 27, 2022.Picha: Pedro Nunes/REUTERS

Taka za palstiki zilizopatikana ndani ya samaki kwenye kina kirefu cha  bahari,zinakadiriwa kuua zaidi ya mamilioni ya ndege wa baharini na pia viumbe wa  majini zaidi ya millioni  kila mwaka. 

Suluhisho ni kufikia viwango vya kimataifa vya kuchakata na uzalishaji wa plastiki. Uvuvi wa kimataifa pia utaangaziwa  katika mkutano huo wa siku tano, unaohusu bahari,ulioandaliwa na Umoja wa mataifa.    

 "Theluthi moja ya hifadhi ya samaki mwitu wamevuliwa kupita kiasi na chini ya asilimia 10 ya bahari inalindwa," Kathryn Matthews, mwanasayansi mkuu wa shirika lisilo la kiserikali lialoshughulikia masuala ya bahari yenye makao yake  nchini Marekani ya Oceana, aliiambia shirika la habari la  AFP.

Wafahamu vijana wanaharakati wa mazingira Ghana

 "Meli na za uvuvi haramu zinafanya kazi bila kuthibitiwa kwenye  maji mengi ya pwani na  bahari kuu."Mkutano huo pia utajadili jinsi ya kusitishwa kwa uchimbaji wa madini katika kina kirefu cha bahari.Wanasayansi wanasema mifumo ikolojia ya chini ya bahari ni dhaifu na inaweza kuchukua miongo kadhaa au zaidi ili kutengamaa..

(Reuters)