UN yaidhinisha marufuku ya ndege kuruka Libya | Habari za Ulimwengu | DW | 18.03.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

UN yaidhinisha marufuku ya ndege kuruka Libya

Baraza la Usalama la umoja wa mataifa limeidhinisha azimio la kuiwekea Libya marufuku ya ndege kuruka kwenye anga yake baada ya kukihitimisha kikao chake cha dharura.

default

Kikao cha Baraza la Usalama la UN

Kulingana na azimio hilo,jamii ya kimataifa ina uwezo wa kufanya kila iwezalo kuishinikiza marufuku huyo itimizwe ila haliruhusu uvamizi wa moja kwa moja kwenye ardhi ya Libya.Hatua hiyo imezua hisia tofauti katika jamii ya kimataifa.

Flash-Galerie UN Libyen Diplomatie Flugverbotszone

Urusi(pili) kutoka shoto haikulipigia kura azimio la kuiwekea Libya vikwazo vya angani

10 kwa 5

Azimio hilo,1973, liliidhinishwa na mataifa 10 kati ya yote 15 wanachama wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa.Ifahamike kuwa matano yaliyosalia hayakushiriki katika zoezi hilo.Orodha ya mataifa hayo inayajumuisha Ujerumani,China,Urusi,Brasil na India.Kwa upande wake,Marekani imefurahishwa na matokeo ya azimio hilo lililo na azma ya kuyadhibiti mashambulio ya angani.Balozi wa Marekani katika Baraza  la Usalama la Umoja wa Mataifa Dr Susan Rice alisisitiza kuwa lengo la hatua hiyo ni kumwasilishia Kanali Gaddafi ujumbe maalum kuwa "Mosi ni kuwalinda raia…kadhalika kuuwekea mbinyo zaidi uongozi wa Kanali Gaddafi pamoja na vikwazo vikali zaidi.Kwa pamoja vipengee hivi vya azimio 1973 vitafanikiwa na sharti vitimizwe na uongozi wa Gaddafi."

Westerwelle Deutschland UN Sicherheitsrat

Guido Westerwelle,Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani

Mashambulio ya angani

Msimamo huo unaungwa mkono na Uingereza,Lebanon na Ufaransa.Kulingana na wanadiplomasia wa Uingereza,Ufaransa na Marekani,vikosi vya Kanali Gaddafi huenda vikashambuliwa kwa anga katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi ya Benghazi.Hata hivyo,viongozi hao wa kimataifa wameyatolea wito mataifa ya Kiarabu kuwaunga mkono katika harakati hizo.Ufaransa iliyokuwa mstari wa mbele kuzipa msukumo juhudi za kuliidhinisha azimio hilo nayo pia imetiwa moyo na matokeo.

EU Gipfel Brüssel Herman Van Rompuy

Herman Van Rompuy,rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya

EU na ushirikiano

Kwa upande wake Umoja wa Ulaya nao pia umeiunga mkono hatua hiyo.Katika taarifa yao ya pamoja,Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya,Herman Van Rompuy,na mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya ,Catherine Ashton,azimio hilo linaipa jamii ya kimataifa fursa ya kuwalinda raia wa Libya kwa kufuata misingi ya sheria.Wanadiplomasia hao wa ngazi za juu wameusisitizia umuhimu wa kushirikiana kwa karibu na Umoja wa Mataifa pamoja na jumuiya mbili zinazoiunga mkono hatua ya kuiwekea Libya marufuku ya ndege kuruka kwenye anga yake,Umoja wa Mataifa ya Kiarabu na ule wa Afrika,AU.Umoja wa Ulaya umeandaa vikao maalum vya majadiliano zaidi kuhusu utekelezaji wa hatua hizo ifikapo tarehe 21 mwezi huu.

Msimamo wa Ujerumani

Hata hivyo Ujerumani ambayo haikulipigia kura azimio hilo, imesisitiza kuwa inaziunga mkono juhudi zote za kuwalinda raia wa Libya ila kamwe haitowapeleka wanajeshi wake kushiriki kwenye operesheni yoyote ile ndani ya ardhi ya nchi hiyo.Waziri wa Mambo ya Nje Guido Westerwelle alifafanua kuwa kuna hatari nyingi na uwezekano wa ajali jambo linaloifanya Ujerumani kutokiunga mkono kipengee hicho.

Luftangriff Rauchwolke Straße Libyen

Hali ilivyo mashariki ya Libya:jambo lililolifanya baraza la usalama la UN kuidhinsha marufuku ya ndege kuruka

Mchango wa nyenzo

Msimamo huo unaungwa mkono na Poland itakayotoa usaidizi kwenye suala la nyenzo.Norway kwa upande wake imeeleza kuwa itashiriki kwenye operesheni hiyo ila haijafafanua kwa njia gani.Denmark nayo inasubiri idhini ya bunge kabla ya kuitoa kauli yake kuhusu suala hilo. 

Ifahamike kuwa  utekelezaji wa azimio hilo utategemea mchango wa zana za angani kwani linayapiga marufuku majeshi yoyote ya nchi kavu kuingia Libya.

Mwandishi:Mwadzaya,Thelma-AFPE/RTRE/APE,UN WEbcasts

Mhariri: Miraji Othman

DW inapendekeza

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com